Na. Faraja Kihongole,Dar es Salaam.
Rais wa marekani Bacrak Obama amewasili nchini kwa
ziara ya siku mbili na ndege ya air force one akitokea afrika ya kusini ambako
alikuwa na ziara ya kikazi na kupokelewa na mwenyeji wake rais Jakaya kikwete.
Rais Obama aliwasili kwenye uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere jijini dar es salaam majira ya saa nane na dakika
37 mchana akiwa amefuata na mkewe pamoja na watoto wake wawili huku ulinzi
ukiwa umeimarika na gari maalumu la kumbeba likiwa pembeni mwa ndege hiyo ya
air force one, na shughuli zote za uwanjani hapo kwa asilimia kubwa zikifanywa
na makachero wa kimarekani.
Baadaye rais Obama akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya
kikwete walipigiwa nyimbo za mataifa haya mawili yaani wa Marekani na ule wa Tanzania ambayo
ilikwenda sambamba na upigaji wa mizinga ishirini na moja.
Rais Obama ( Kushoto) akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya kikwete |
Hatimaye Rais Obama alikagua gwaride aliloandaliwa na
wanajeshi wa jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania
kabla ya kuelekea Ikulu alikoandaliwa mapokezi rasmi
Rais Obama aliangalia ngoma mbalimbali za asili ya kitanzania.
Akiwa nchini rais Obama kesho anatarajiwa kutembelea
ubalozi wa Marekani na kukutana na wafanyakazi
na baadaye atakwenda ubungo kutembelea mitambo ya kufua umeme
inayoendeshwa na kampuni ya symbion ya marekani kabla ya kuondoka kurejea
Marekani.
0 comments:
Post a Comment