Ripoti ya biashara ya dunia ya mwaka 2013 iliyotolewa na Shirika la Biashara Duniani...
imechambua mwelekeo wa biashara ya dunia na athari ya hali ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ya hivi sasa na ya siku zijazo.
Ripoti hiyo inaonesha kuwa, katika miaka 30 iliyopita,
ongezeko la biashara ya kimataifa lilizidi ongezeko la uzalishaji duniani, hasa
lile la nchi zinazoendelea.
Mwaka 1980 mauzo ya bidhaa za China katika nchi za nje
yalichukua asilimia 1 ya mauzo ya bidhaa nje duniani, kiasi hiki kiliongezeka
kuwa asilimia 11 mwaka 2011.
Nchi nne zilizouza bidhaa nyingi zaidi nje duniani
mwaka 2012 zilikuwa China, Marekani, Ujerumani na Japan, na nchi nne
zilizoagiza bidhaa nyingi zaidi kutoka nje zilikuwa Marekani, China, Ujerumani
na Japan.
0 comments:
Post a Comment