Shirika la idadi ya watu la Umoja wa Mataifa
UNFPA limetaka nchi
za Afrika kuongeza
matumizi ya wakunga ili kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.
Ofisa wa Shirika hilo Pulani Tlebere alisema idadi
kubwa ya vifo vya kina mama wanaojifungua na watoto wanaozaliwa barani Afrika
vinatokana na kina mama kujifungua bila kuwepo kwa wataalamu.
Bw. Tlebere amesema kwa sasa ni asilimia 50 tu ya kina
mama barani Afrika wanaojifungua mbele ya wakunga wataalamu.
Waziri wa Afya wa Kenya Bw. James Macharia amesema
wakunga ni watu muhimu sana wakati wa kina mama kujifungua, lakini hali ya
mazingira ya kina mama wa Afrika kujifungua haiboreki.
James Macharia - Waziri wa afya Kenya |
Ametolea mfano
Kenya kuwa kina mama 488 kati ya laki moja wanakufa wakati wa kujifungua.
Kutokana na
hali hiyo Kenya inafanya juhudi ya kupunguza idadi hiyo ili ifikie 155 kabla ya
mwaka 2015 kama inavyotakiwa na malengo ya maendeleo ya Milenia.
0 comments:
Post a Comment