Aliyekuwa Waziri Mkuu
wa Tanzania Mheshimiwa Edward Lowassa, amemsifia
Rais Jakaya Kikwete kuwa ameweza kuifanya Tanzania kupata
heshima katika ulingo wa kimataifa.
Kaulihiyo ameitoa wakati akihojiwa
na Swahili TV jijini Washington DC.
Alisema kitendo cha
Rais wa Marekani Bwana Barack Obama kuja nchini na sambamba na viongozi mbalimbali
wa mataifa makubwa kumeonyesha jinsi gani Rais kikwete anavyokubalika katika mataifa ya wenzetu.
“Ni hivi
karibuni tu Rais Xi Jinping wa China, Rais Obama na Rais
mstaafu wa Marekani George W.Bush walikuwa nchini
Tanzania, hii inaonyesha kuwa Tanzania iko juu katika medani za kimataifa”
alisema Lowassa.
Aidha Lowassa
ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara ya kikazi, aliongeza kwa kusema,
Rais Kikwete anastahili pongezi sana kwa hilo kwani sio rahisi kwa
viongozi wa mataifa makubwa kutembelea nchi zingine labda kama mko juu
sana katika medani za kimataifa.
alisema
Rais Kikwete amekuwa akihusishwa na utatuzi au ushauri wa kutatua
matatizo mbalimbali ya nchi zingine na pia ameanza kuishirikisha Tanzania
katika usimamizi wa amani katika nchi mbalimbali.
Tanzania iliweka
historia hivi karibuni kwa maraisi wawili wa Marekani kukutana katika
nchi moja kwa wakati mmoja, Rais Barack Obama na George W.Bush walikutana
jijini Dar es Salaam mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment