Na Boniface Wambura, TFF.
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini
Tanzania (TFF) limemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Bernard Luanda kwaajili ya
kuongoza Kamati ya Rufani ya Uchaguzi kufuatia mabadiliko ya Katiba
yaliyofanywa Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) na kuingiza kamati nyingine mpya.
Kauli hiyo imetolewa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga ambapo
ametangaza wajumbe wa kamati hizo hii leo mara tu baada ya kikao
cha Kamati ya Utendaji ya TFF kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema uteuzi wa wajumbe
hao umezingatia maoni ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, lakini vilevile
amewashukuru wajumbe walioteuliwa kwa kukubali kutoa mchango wao katika maendeleo
ya mpira wa miguu nchini.
Mbali ya Jaji Luanda ambaye
ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, wajumbe ni Francis Kiwanga (Makamu Mwenyekiti),
Anney Semu, Yohane Masalla na Allen Kasamala. Kamati ya Uchaguzi inaongozwa na
Hamidu Mbwezeleni, Moses Kaluwa (Makamu Mwenyekiti), Mustafa Siyani, Hassan
Dyamwale na Kitwana Manara.
Mwenyekiti Kamati ya Rufani
ya Maadili ni Jaji Steven Ihema, Bi. Victoria Makani (Makamu Mwenyekiti),
Mheshimiwa Mohamed Missanga, Henry Tandau na Mheshimiwa Murtaza Mangungu.
Kamati ya Maadili inaundwa na Bi. Jesse Mguto (Mwenyekiti), Francis Kabwe
(Makamu Mwenyekiti), Profesa Mtambo Madundo, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP)
Mohamed Mpinga na Evod Mmanda.
Profesa Mgongo Fimbo
anaongoza Kamati ya Rufani ya Nidhamu wakati Makamu wake ni Ong’wanuhama Kibuta
na wajumbe ni Kanali Mstaafu Idd Kipingu, Dk. Mshindo Msolla na Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Mstaafu Jamal Rwambow. Kamati ya Nidhamu
inaongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) Mstaafu Alfred Tibaigana, Mustafa Kambona
(Makamu Mwenyekiti), Mheshimiwa Azzan Zungu, Yusuf Nzowa na Mohamed Msomali.
Pia Kamati ya Utendaji
imefanya mabadiliko katika Kamati ya Waamuzi ambapo Said Nassoro na Charles
Ndagala kutoka Chama cha Waamuzi wanachukua nafasi za Joan Minja na Riziki
Majala. Kamati hiyo inaendelea kuongozwa na Kapteni Mstaafu Stanley Lugenge,
Omar Kasinde (Makamu Mwenyekiti) wakati mjumbe mwingine ni Mohamed Nyama.
0 comments:
Post a Comment