M23 |
Mwanaharakati mmoja wa
kutetea haki za binadamu amesema kuwa, waasi wa M23 wanazitishia familia za
wahanga ambao walioko kwenye mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na
Rwanda wasitoe taarifa zozote zilizokuwa dhidi yao kwa shirika la kutetea haki
za binadamu la Human Rights Watch.
Mwanaharakati huyo ambayo hakuwa tayari
kujitambulisha wasifa wake amesema kuwa, waasi wa M23 wamekuwa wakizituhumu
familia za wahanga kwa kutoa taarifa zao kwa shirika hilo la kutetea haki za
binadamu.
Shirika la Human Rights Watch hivi karibuni
lilitoa taarifa na kueleza kuwa, waasi wa M23 walioko mashariki mwa Kongo
waliwahukumu adhabu ya kifo watu 44 bila ya kuwafungulia mashtaka katika jimbo
la Kivu Kaskazini mashariki mwa Kongo, kwa makosa ya kuwabaka wanawake na wasichana
61 na kuwafanyisha kazi kwa nguvu watoto wadogo.
Wakati huohuo, waasi wa M23 wanawashikilia
vijana wasiopungua 50 kwa tuhuma za kushiriki kwenye maandamano yaliyopelekea
kuchomwa moto maduka ya watu wanaozungumza lugha ya Kinyarwanda huko mashariki
mwa Kongo. Hayo yameelezwa na Luteni Kanali Vianney Kazarama Msemaji wa kundi
la waasi wa M23.
0 comments:
Post a Comment