Image
Image

MAAJABU: HAWA NDIO WACHINA AMBAO WAMEVUNJA REKODI YA KUWA NA JENGO KUBWA KULIKO YOTE DUNIANI.

Sehemu ya ndani
Sehemu ya muonekano wa jengo hilo.
Mandhali ya jengo hilo jinsi yavyoonekana.

CHINA wafungua jengo kubwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wake, Jengo hilo kubwa kuliko yote duniani lina Urefu wa Ghorofa 18 Tu, Kama letu la Benjamin Mkapa Pension Towers uongeze na ghorofa 3 hivi juu.

Ukubwa wa jengo hili ni kutokana na upana wake ambao unafikia Kilomita za Mraba Milioni 1.2, Jengo hili lipo huko Chengdu, kwa ukubwa wake zinaweza kuingia Pentagon 3 za wamarekani, Miji minne (4) ya Vatican na zaidi ya nyumba 20 za Sydney Opera.

Jengo hilo lina maduka kadhaa ya kufanyia shopping za mahitaji mbali mbali, na Hotel kubwa za hadhi ya Nyota 5 mbili, kila moja ikiwa na vyumba 1,000.

Mbali na hayo jengo hilo lina mandhari nzuri kwa nje kuanzia pools na bustani huku kukiwekwa mitambo maalum ya jua la kutengeneza ili kutoa kivutio katika hizo pools. Kwa hesabu za sasa jengo hilo ni kubwa kuliko viwanja 329 vya mpira wa miguu vikiwekwa pamoja.

Uzinduzi rasmi wa jengo hilo unatarajia kufanywa mnamo August 22 mwaka huu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment