Ernest Mangu - Kamanda wa polisi Mwanza. |
Siri
za wizi uliotokea Makao Makuu ya Polisi mkoani Mwanza zimeanza kuvuja ambapo
imebainika kuwa kompyuta aina ya laptop zilizoibwa ndani ya chumba cha
vielelezo zilikuwa za ushahidi wa kesi ya wezi wa mashine za kuchukulia
fedha(ATM).
Katika
wizi huo wa benki ambao ulifanyika kwenye mashine za ATM mbalimbali na
watuhumiwa watatu kunaswa Februari 10, mwaka huu saa 6 usiku wakiiba kwenye ATM
za NMB,Tawi la PPF Plaza, Polisi walinasa vitu vingi vya watuhumiwa
hao ikiwa ni pamoja na kompyuta mbili ambazo zinadaiwa kuibwa kituoni hapo
juzi.
Habari zilizopatikana kutoka ndani ya
Polisi zimeeleza kwamba katika wizi huo uliotokea katika maghala ya Polisi,
moja kati ya vifaa vilivyoibwa ni mafaili mbalimbali ya vielelezo kadhaa vya
kesi zinazochunguzwa na polisi ikiwa ni pamoja na laptop hizo ambazo zilikuwa
ni ushahidi kwa kesi hiyo ya wizi wa ATM.
Kamanda
wa Polisi mkoani Mwanza, Ernest Mangu alipoulizwa kuhusiana na vielelezo
vilivyoibwa Polisi, alikanusha kwamba laptop hizo zilikuwa kielelezo cha kesi
za wizi wa fedha katika ATM lakini pia hakuwa tayari kueleza zilikuwa za kesi
gani
Wakati
Kamanda huyo akikanusha baadhi ya askari ambao wanahusika na uchunguzi huo
wamedai kuwa wizi huo uliendeshwa na maofisa wa polisi wasio waaminifu na
kubainisha hakuna wizi unaoweza kufanywa na watu kutoka nje ya polisi.
0 comments:
Post a Comment