Hatimaye miili ya wanajeshi saba wa jeshi la
Tanzania JWTZ waliokuwa katika ulinzi wa
amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan imewasili jana nchini na ndege maalum
ambapo makamu wa rais Dk Mohammed Gharib Bilal amewaongoza waombolezaji kupokea
miili hiyo.
Katika uwanja
ndege wa jeshi la anga jijini Dar
es salaam ndugu, jamaa na marafiki wa familia za marehemu pamoja na viongozi
mbalimbali wa serikali akiwemno Mkuu wa majeshi ya ulinzi Davis Mwamunyange,
mkuu wa jeshi la polisi IGP Said Mwema, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck
Sadick walishiriki kupokea marehemu hao waliouawa tarehe 13 Julai mwaka huu.
Kaimu mkurugenzi wa habari jeshini Meja Joseph Masanja
amewaambia waandishi wa habari uwanjami hapo kuwa miili hiyo imepelekwa katika
hospitali ya jeshi lugalo kabla ya kuagwa rasmi katika viwanja vya wizara ya
ulinzi na jeshi la kujenga taifa Upanga
jijini Dar es salaam.
Hata hivyo siku
ya jumatatu Julai 22 majira ya asubuhi
heshima zote za kijeshi zitatolewa na baadae kusafirishwa kupelekwa ambako
miili itazikwa.
Meja Masanja alisema miili iliyopokelewa uwanjani hapo
ni ya Koplo Muhamed Juma Ali, Koplo
Muhamed Chukilizo, Private Rodney Msofe, Private Fortunatus Msofe, Sajenti
Shaibu Othamn, Koplo Osward Chaula na Private Petter Werema.
Aidha Tayari Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Rais Jakaya Kikwete amekwishafanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Sudan Omar Bashir kufuatia kuuawa na kujeruhiwa kwa askari wa Tanzania, walioko katika ulinzi wa kimataifa wa amani katika jimbo la Darfur na kumtaka Rais huyo kuchukua hatua za haraka kuwasaka na kuwakamata wale wote waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha mbele ya sheria haraka iwezekanavyo.
Jakaya Kikwete- Rais wa Tanzania |
Omar Bashir - Rais wa Sudan. |
0 comments:
Post a Comment