Image
Image

MADELA HATIMAYE ATIMIZA MIAKA 95 YA KUZALIWA KWAKE.



Rais wa zamani wa Afrika Kusini mzee Nelson Mandela ametimiza miaka 95, akiwa amelazwa hospitalini kwa muda wa wiki sita sasa.

Ikulu ya nchi hiyo imesema hali ya mkongwe huyo inaonyesha kuboreka kidogo. 

Salamu zimemiminika kumpongeza mzee Nelson Mandela na kumtakia nafuu ya haraka.
Rais Barack Obama wa Marekani amesema katika salamu zake kwamba yeye na familia yake walitiwa hamasa na ushujaa wa Mandela, baada ya kutembelea gereza alikofungiwa kwa miaka mingi wakati wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Mapema leo Ikulu ya Afrika Kusini imetoa tangazo linaloarifu juu ya afya ya mzee Mandela.

 ''Madiba anabakia hospitalini mjini Pretoria, lakini madaktari wanaomtibu wanathibitisha kuwa hali yake inaboreka taratibu'', lilisema tangazo hilo, likitumia jina la kiukoo la Mandela..Madiba.

Mbali na kumpongeza Mandela kwa kutimiza miaka 95, Rais Obama ametoa wito kwa watu kuadhimisha siku ya Mandela wafanya kazi za kujitolea kwa kuenzi jina lake.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment