Watata; Viongozi wa
Yanga SC, kutoka kulia Balozi Ammy Mpungwe, Mjumbe Baraza la Wadhamini,
Mwenyekiti wa klabu, Yussuf Manji, Waziri George Mkuchika, Mwenyekiti Baraza la
Wadhamini, Francis Kifukwe, Mjumbe Baraza la Wadhamini na Clement Sanga, Makamu
Mwenyekiti wa klabu .
YAH: URUSHWAJI KATIKA
TELEVISHENI MICHEZO YA YANGA.
“HIVI karibuni,
Tanzania Football Federation (TFF) iliunda Tanzania Premier League chini
ya Bodi yampitoBodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo Bodi itakayokuwa
imechaguliwa kidemokrasia.
Bodi hii imeamua peke yake kuingia katika mkataba wa
miaka 3 (mitatu) na kampuni inayoitwa Azam Television (ambayo ina
mapromota wale wale wanaomiliki Azam Football Club).
Makubaliano ambayo
Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam Television, Kamati ya Utendaji ya YANGA
inalipinga kwa nguvu zote katika misingi ifuatayo:
1. BODI YA TPL.
1.1 Bodi iliyoko sasa
hivi ni ya mpito ambayo ilitakiwa kutenguliwa na Bodi iliyochaguliwa
kidemokrasia kwa kupitia uchaguzi wa tarehe ……….. mwaka huu na haitakiwi
kuingia katika mikataba a miaka mingi wakati inakaribia kuondoka katika ofisi.
1.2 Bodi ya TPL
iliyoko sasa hivi haikuchaguliwa kidemokrasia.
1.3 Bodi ya TPL
iliyoko sasa hivi haina mjumbe hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA.
2. UTARATIBU WA DUNIA
NZIMA.
2.1 Haijawahi kutokea
katika ligi ya mpira wa miguu ya kisasa kulazimishwa kwa Klabu inayoshindana
katika ligi kuachia haki zake za urushwaji wa michezo zichukuliwe na chombo cha
habari cha Klabu ya upinzani.
2.2 Mfumo
(undertaking) ambao TPL inataka kuanzisha kwa njia ya kulazimisha mkataba kwa
YANGA iachie urushwaji wa michezo yake ya soka yarushwe na Azam TV
unatishia sana uwepo wa msingi wa ushindani katika soka ya Tanzania.
2.3 Makubalianokati ya
TPL na Azam Television kuhusu utaratibu wa malipo yanasemakwamba Klabu ya YANGA
na Klabu zingine zitakazoshiriki katika Ligi Kuu ya Tanzania watapata
mgao sawa wa mapato ya urushwaji wa michezo hii, ambayo YANGA inapinga kwa
sababu kama inavyofanyika duniani kote kwenye ligi zilizofanikiwa (angalau)
kutofautisha mgawanyo wa mapato kati ya timu kufuatana na matokeo ya mwisho wa
ligi.
2.4 Kamati ya Utendaji
ya YANGA siyo tu haikubaliani na mgawanyo sawa wa mapato ambao hautofautishi
kati ya timu ya kwanza katika ligi na timu ya mwisho katika ligi, lakini pia
ukosefu wa viwango (premiums) vitakavyolipwa:
2.4.1 Vilabu vya mpira
vyenye ufuasi wa washabiki wengi;
2.4.2 Vilabu vya mpira
vinavyoendeshwa na Wanachama;
2.4.3 Vilabu vya mpira
visivyopata ruzuku kutoka Serikalini n.k.
3. MIGOGORO YA MASLAHI.
3.1 Makamu Mwenyekiti
wa Bodi ya Mpito ya TPL ni Mkurugenzi mwandamizi wa Makampuni ya Azam na
kwa hivyo mazungumzo ya siri kati ya Bodi ya TPL na Azam ni ya kutiliwa
mashaka.
3.2 Makampuni ya Azam
yana yanashindana kibiashara na makapuni mengi yakiwemo ya utengenezaji wa
vinywaji baridi na imeonyesha huko awali inaweka “matakwa maalum” muhimu zaidi
kuliko mprira wa miguu, kama vile Azam F.C.hawashiriki katika Kombe la
Tusker na kwa hiyo YANGA inakuwa na msimamo kwamba kwa Azam Television kupewa
leseni ya kurusha matangazo ya mpira wa miguu inatishia biashara za washiriki
wa sasa na wa baadaye wa YANGA.
3.3 Azam na YANGA wana
uadui wa kimichezo. Kumbuka, wakati MRISHO NGASSA alipotaka kwenda YANGA, Azam
F.C. walimkopesha kwa nguvu kwa Klabu ya Simba! Kwa hiyo YANGA itahatarika kwa
matangazo yenye upendeleo kama Azam Television itarusha hewani michezo yake
n.k.
4. KUTOKUWA NA UWAZI.
4.1 Mkataba wa
utangazaji wa miaka mingi unaotaka kuingiwa kati ya TPL na ambao
badohaujarushwa Television ya Azam haukushindanishwa na vyombo vingi vya
habari, na vyombo ambayo wako tayari kwenye soka havikujulishwa kuhusu
fursa hii au walizuiliwa kufikisha mapendekezo yao ya maombi ya haki za kurusha
matangazo katika Ligi Kuu (Tanzania Premier League).
4.2 Ukosefu wa uwazi
wa TPL unanonyesha kuwa MoU iliyokusudiwa kuwekewa saini na TPL haikufikishwa
YANGA kwa ajili ya mapitio ya kisheria, licha ya YANGA kufanya ombi hilo
kwaTPL.
5. MAZINGATIO YA
KIBIASHARA.
5.1 Mamlaka ya kuamua
mzozo wowote wa mkataba wa leseni ya utangazaji wa Ligi Kuu (Tanzania Premier
Leagu) itakuwa ni Mahakama ya kisheria na siyo FIFA. TPL inasingizia
kwamba leseni ya matangazo ambayo inakusudia kufanya kuwa ni maagizo ya
FIFA na kwa hiyo YANGA inapaswa kuukubali "lock, stock and barrel."
5.2 TPL inaelezea
kimakosa makubaliano ya leseni ya urushaji wa mchezo ya mpira
inayotarajia kuingia na Television ya Azam kama "makubaliano ya
udhamini" (“sponsorship agreement”) ambayo siyo sahihi, kwa sababu
urushaji wa michezo ya mpira wa miguu ni biashara inayotokana na maslahi ya
uhusiano na hivyo wahusika wote ni
lazima wazingatie maslahi yao ya kifedha.
Kwa mfano, moja ya
vyanzo muhimu vya mapato ya YANGA ni mapato ya kiingilio ya mlangoni yatokanayo
na michezo ya mpira wa miguu ambayo urushwaji wa michezo hii itapunguza mapato
haya. Kwa wastani michezo ya YANGA Dar es Salaam huingiza makusanyo ya
mlangoni shilingi milioni 50 kwa kila mchezo na hata kushuka kidogo kwa 25%
katika mahudhurio ya mechi za YANGA zinafikia mara mbili ya mapendekezo ya
mapato takribani Sh milioni 8.3 kwa mwezi kupokelewa na YANGA kutoka mradi wa
kibiashara kati ya TPL na Azam Television. Kwa kuzingatia haya, kwamba hata
siku za nyuma kama kulikutokea fursa ya kurusha mchuano wa mpira unapochezwa,
wadau wote (Timu za mpira wa miguu, TFF na Mtangazaji) walikuwa
wanaafikiana kwanza kwa pamoja kuhusu mapato na mgawanyo wake.
Kamati ya Utendaji ya
YANGA ina maoni kwamba makubaliano yoyote ya kibiashara yanayoihusu ni lazima
iyalinde maslahi kifendha ya Klabu yake ambapo makubaliano ya TPL / Azam
Television hayaangalii na kwa hiyo, Kamati ya Utendaji ya YANGA haitaki mchezo
wake urushwe hewani na Azam Television.
Msisitizo wa TPL kuwa
lazima Azam Television irushe hewani michezo ya YANGA linasikitisha. Kamati ya
Utendaji ya YANGA haina tatizo na Vilabu vingine vya mpira wa miguu zikiruhusu
michezo yao kurushwa na Azam Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha
YANGA kuonyesha mchezo wake wa Vodacom Premier League katika Azam Television.
(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI
YOUNG AFRICANS SPORTS
CLUB
29 JULAI, 2013
0 comments:
Post a Comment