Baadhi ya waandishi waliotunukiwa tuzo ya uandishi bora wa usalama barabarani.
Taasisi ya Automobile
Association Tanzania (AAT) imetoa tuzo kwa waandishi wa habari kutoka
katika vyombo vya mbalimbali vya habari walio shiriki katika kutoa
habari kwa wananchi kuhusu mafunzo yalio tolewa kwa waendesha bajaji na
pikipiki 2500 kuhusu matumizi salama ya barabara.
Tuzo hizo zimetolewa
leo pamoja fedha taslimu na Rais wa taasisi hiyo Bw.Nizar Jivan
katika sherehe fupi ilio fanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar
es Salaam,Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wamewaza
kujinyakulia tuzo hizo.
Rais huyo
alitoa tuzo hizo kwa waandishi na watu waliosaidia
kukamilisha mafunzo hayo, ambapo miongoni mwao ni
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw.Assa Mwambene, ambaye tuzo yake
ilikabidhiwa kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo,
Zamaradi Kawawa.
Wengine waliopata tuzo hizo
ni Mohamed Ugassa kutoka gazeti la The Guardian,Freginia Ole Swai kutoka
ITV,Fred Mwanjara wa Channel Ten,Elias Shamt wa TBC,Miguel Suleiman wa
Citizen,Nasongelya Kilyanga wa Daily News,Khadija Mussa wa gazeti wa
Uhuru,Zainabu Malongo kutoka Mwananchi,Hadja Hamis kutoka Mtanzania,Abas Yusuph
mwandishi wa kujitegemea,Judica Benedict wa The Guardian.
Akizungumza na waandishi wa
habari katika sherehe hiyo Bw.Nizar amesema kuwa,anawashukuru waandishi wa
habari kwa kusaidia kutoa habari kwa wananchi juu ya mafunzo hayo yalio husisha
matumizi salama ya barabara na jinsi ya kuepusha ajali za barabarani.
Vilevile taasisi hiyo
imeitaka Serikali kuweka mikakati madhubuti ambayo itarahisisha kupambana na
matumizi mabaya ya barabara.
“Serikali ihakikishe bodaboda
zote zipewe namba maalumu ili iwe rahisi huzitambua pindi uhalifu utakapotokea
kama ilivyo kwa teksi,” alisema Jivan.
Naye mmoja wa waandishi wa habari
aliyejinyakulia tuzo hizo , Ugassa kutoka gazeti la The Guardian,ametoa wito
kwa waandishi wa habari kuzidisha uhamasishaji dhidi
ya matumizi bora ya barabara na kulipa mkazo suala hilo kama
wafanyavyo katika masuala mengine kama vile Ukimwi.
0 comments:
Post a Comment