Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametembelea eneo
lililokumbwa na maafa mwishoni mwa wiki, kufuatia moto mkubwa uliowaka katika
magari yenye matanki ya mafuta ambapo
idadi ya watu waliopoteza maisha imefikia 35.
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini humo, Rosemary
Namayanja amesema miili kumi na saba imepatikana eneo la tukio, miili mingine
imeshindwa kutambulika kufuatia kuharibika vibaya, hatua iliyolazimu kuzoa mavumbi yaliyosalia.
Ajali hiyo ilitokea eneo la Namungoona, Kaskazini mwa
Uganda baada ya gari moja aina ya Noah kugongana na gari kubwa iliyokuwa
imebeba mafuta ya Petrol.
0 comments:
Post a Comment