Baada ya kipindi cha miaka 39 baadhi ya watoto wa
wajenzi wa reli ya Tazara kutoka China, wameweza kupata nafasi ya kutoa heshima
zao kwa wazazi wao ambao walifariki wakati wanashiriki ujenzi wa reli hiyo
miaka ya mwishoni mwa sitini, shughuli ambayo ilifanyika katika eneo yalipo
makaburi hayo,Ukonga,Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Watoto wa wajenzi wa reli ya Tazara kutoka China wakionekana kwa staili tofauti wakati wakifanya kumbu kumbu ya kuwakumbuka wazazi wao waliofariki. |
Huku wengi wao wakibubujikwa na machozi kwa kuyaona
makaburi ya baba zao kwa mara ya kwanza, waliweza kuweka mashada ya maua na
vitu mbalimbali vinavyoambatana na desturi ya dini zao ikiwemo kuweka matunda,
biskuti, keki na kuwasha sigara tatutatu kila kaburi.
Hapo jana wakikaribishwa na balozi wa china hapa
nchini, Lu Yu shing, ambae alielezea namna nchi yake ilivyojitoa muhanga wakati
ule wa kujitosa kuzisaidia nchi za Zambia na Tanzania kwa kujenga reli hiyo kwa
msaada wa dola milioni 500, aliwataka wafiwa hao kuwa na faraja, kwamba wazazi
wao walikufa huku wakitekeleza kitendo cha kishujaa.
0 comments:
Post a Comment