Rais Barack Obama wa Marekani anaanza ziara ya kiserikali nchini Tanzania
ambayo itamchukua siku mbili.
Rais huyo wa taifa kubwa lenye nguvu kiuchumi duniani,
anatarajiwa kuwasili majira ya saa nane mchana, baadaye kufanya mazungumzo na
Mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimeimarisha ulinzi kila
mahali, kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, barabara
atakazopita hadi Ikulu pamoja na kwenye miradi atakayotembelea ukiwemo Mradi wa
kufua Umeme wa Symbion uliopo Ubungo Tanesco.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amewaomba wakazi wa Jiji
kujitokeza kwa wingi kumlaki kiongozi huyo ambaye anafanya ziara ya kihistoria
nchini Tanzania, ziara ambayo inatarajiwa kuwa na mafanikio makubwa ya
kiuchumi.
0 comments:
Post a Comment