Polisi nchini marekani ikiwa imemshikilia moja ya mtuhumiwa wa vitendo vya ubakaji na ukahaba nchini Humo.
Polisi nchini Marekani imewatia mbaroni watu 150 kwenye
oparesheni ya kupambana na vitendo vya ukahaba na ubakaji dhidi ya watoto
nchini humo.
Polisi huko nchini Marekani imeeleza kuwa, watu hao 150 walitiwa mbaroni katika
miji 76 ya nchi hiyo kwa tuhuma za kuwanajisi na kuwabaka watoto.
Oparesheni
hiyo ilifanikiwa kuwakusanya watoto 105 waliokutwa kwenye vituo vya malori,
hoteli mbalimbali, kumbi za starehe na kwenye makasino.
Vitendo vya ubakaji na
udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto, ni moja kati ya jinai kubwa zinazofanywa
nchini Marekani. Imeelezwa kuwa, kiwango kikubwa cha watoto wenye umri wa
miaka 13 hadi 16 huwa wahanga kwa kutumbukia kwenye vitendo hivyo vilivyo
kinyume cha maadili ya mwanadamu.
0 comments:
Post a Comment