Baadhi ya wanachama wa klabu ya Simba ya
Dar Es Salaam wameondoka katika mkutano wao mwaka uliofanyika katika ukumbi
wa maafisa wa polisi Oysterbay,wakidai
kutoelewa umuhimu wake kutoka na madai kwamba hakuna ajenda yenye tija
iliyozungumzwa katika mkutano huo.
Mkutano huo pamoja na mambo
mengine,ulikuwa ujadili mapato na matumizi, uliingia dosari baada ya kuibuka
kwa fujo za hapa na pale kufuatia baadhi
yao kuanza kupinga taarifa ya mpango mkakati wa maendeleo wa klabu hiyo
uliondaliwa na wasomi ikiwa ni sehemu ya
kuuzindua.
Aidha Wanachama hao walipaza sauti huku
wengine wakidai kutotaka kusikia chochote zaidi ya matokeo mazuri ya timu yao.
Awali Mwenyekiti wa Simba Ismael Aden Rage,mbali na kuelezea mafaniko
na ikiwemo ya kuuza wachezaji na kipato chake kuingizwa ndani ya klabu
hiyo,alitumia pia fursa hiyo kupiga vijembe kwa baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa
ni mahasimu wake.
Mkutano mwingine wa dharura kwa mujibu
wa Rage, aliyekubali marekebisho ya katiba ya klabu hiyo,utafanyika Novemba
mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment