WIMBI la majambazi kujitokeza kuteka magari na kuwapora wasafiri limechukua sura mpya baada ya kuanza kuvamia vituo vya polisi kama ilivyoripotiwa jijini Dar na sasa ni Mwanza.
Jijini Mwanza, majambazi yamevamia makao makuu ya polisi na kuiba vielelezo kadhaa ikiwamo begi na laptop.
Baada ya kupekua na kutokuona cha maana kwao, wakatoboa tena dali na kutokea chumba cha tatu ambako walichukua laptop na begi iliyokuwa na vielelezo mbalimbali. Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza ndugu Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisema wahusika hawajakamatwa.
Naye Kaimu Mkaguzi Mkuu wa kanda amekiri kupokea taarifa ya tukio hilo na kuomba wananchi kushirikiana na maofisa wa polisi kuwabaini wahalifu.
Kuhusu TAMBARARE HALISI
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment