Wanajeshi wa DRC wakiwa wamemfunga mpiganaji wa kundi la M23 nyuma ya gari na kumpitisha mitaani. |
Maiti ya muasi wa M23 ikinajisiwa na Askari wa Congo, baada ya kukamatwa, kuteswa hadi kufa katika mapigakano yanayoendelea maeneo ya Kivu na Goma nchini Congo. |
Wanajeshi wa DRC wakiendeleza mateso makali kwa waasi wa kundi la M23 mpaka kifo kinapowafika wakiwa uraiani |
Wanajeshi wa DRC wakiinajisi maiiti ya muasi wa M23 baada ya kukamatwa na kupigwa hadi kufa mbele ya raia. GOMA-DRC. |
WAKATI mapigano yakizidi kuwa makali kati ya
wanajeshi wa DR Congo (FARDC) na kundi la waasi wa M23, wanajeshi wa DRC wako
hatarani kushitakiwa kwa tuhuma za kuwatesa waasi na kunajisi maiti zao.
Wanajeshi hao wanatuhumiwa kwa kosa la
kukiuka haki za binadamu na sheria za Umoja wa Matifa (UN) inayokataza
ukiukwaji wa haki za binadamu huku ukikataza watuhumiwa na mateka wa kivita
kufanyiwa vitendo vyovyote vinavyo ashiria kukiuka haki zabinadamu badala yake
mateka wote wanatakiwa kushtakiwa kwa muujibu wa sheria.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN Ban Ki-moon
alisema kwamba, Umoja huo umeonyesha wasiwasi kuhusu taarifa ya
kutokutendewa haki kwa wafungwa wa M23 na kunajisiwa kwa maiti ya wapiganaji wa
M23 baada ya kukamatwa na vikosi vya silaha.
Wanajeshi wa DRC wakimtembeza muasi wa kundi la M23 mitaani baada ya kukamatwa.
|
Alisema watuhumiwa wa M23 walifanyiwa vitendo
vibaya na askari wa DRC mbele ya raia bila ya kuzingatia Sera ya Umoja wa
Mataifa ya Haki za Binadamu na kwamba watuhumiwa waliohusika katika matukio
hayo watafanyiwa uchunguzi wa kina.
0 comments:
Post a Comment