Mkurugenzi wa Usalama
wa Chadema, Willifred Lwakatare akizungumza kuhusu hali ya ugonjwa wake akiwa
katika Tasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) jijini Dar es Salaam jana.
|
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imempa kibali Mkurugenzi wa
Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred
Lwakatare, akatibiwe nje ya nchi.
Lwakatare
ambaye anasumbuliwa na maumivu ya shingo, kwa sasa amelazwa katika Taasisi ya
Mifupa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) kwa uangalizi maalumu na
kufanya mazoezi, alipata kibali hicho kwa kuwa anakabiliwa na kesi ya kula
njama za kumdhuru Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.
Wakili
wake, Nyaronyo Kicheere alililiambia gazeti hili nje ya mahakama kuwa Lwakatare
anatarajiwa kupelekwa India, lakini akasema tarehe ya kusafirishwa inategemea
na kukamilika kwa taratibu za hospitali alikolazwa, na kule anakopelekwa.
Mahakama
hiyo ilitoa kibali ili akatibiwe nje ya nchi, baada ya Kicheere, kuiomba
mahakama hiyo impe kibali ili akatibiwe nje kama
ilivyopendekezwa na madaktari wake.
Akizungumza
na gazeti hili, Lwakatare alisema ingawa yupo katika uangalizi maalumu, lakini
amefikia uamuzi huo aliosema umekuja baada ya kujadiliana na madaktari
wanaomuhudumia.
“Bado
nafanya mazoezi, lakini kulingana na hali ilivyo imebidi nikae na madaktari
nikashauriana nao nimewaomba niende nje ya nchi nikatibiwe kama
itawezekana,”alisema Lwakatare.
Alisema
pamoja na maombi hayo pia alikuwa anategemea kupata ruhusa kutoka mahakamani
kwa sababu jana ilikuwa tarehe ya kuendelea kutajajwa kwa kesi yake baada ya
kuachiwa kwa dhamana.
Alisema
madaktari wanajaribu kufanya uchunguzi kwa kuzingatia uzoefu wao wao.
Awali
aliwekwa katika Kitengo Maalumu cha Uangalizi wa madaktari na mazoezi kwa muda
wa siku nne madaktari walimtaka kufanya mazoezi kwa saa tatu kwa siku ili aweze
kupona tatizo hilo kabla kufikia hatua ya upasuaji.
Lwakatare
ameomba kwenda kutibiwa nje ya nchi baada ya kukaa muda mrefu hospitalini hapo
bila mabadiliko yoyote.
Lwakatare
alifika Muhimbili Julai 10 kufuatia maumivu ya shingo ambayo chanzo ni chake ni
ajali ambayo iliipata mwaka 2002.
Mbali
na maombi ya kibali cha Lwakatare kwenda kutibiwa nje ya nchi, Wakili Nyaronyo
pia aliiomba mahakama hiyo imchukulie hatua mshirika wa Lwakatare kwenye kesi
hiyo Ludovick Joseph Rwezaura kwa kosa la kuandika makala kwenye mitandao ya
kijamii, akilenga kujitetea dhidi ya shtaka linalomkabili na Lwakatare.
0 comments:
Post a Comment