Serikali imesema inaendelea kupokea
mapendekezo kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuona jinsi ya kupunguza makali ya
Kodi ya shilingi elfu moja kwenye 'sim card' hususan kwa wananchi wa kipato cha
chini.
Waziri wa Fedha, Dk.William Mgimwa
amesema nia ya serikali ni njema na kwamba kodi hiyo inalenga kuboresha huduma
ya maji umeme na barabara vijijini.
Dk.William Mgimwa - Waziri wa fedha Tanzania. |
Dk.Mgimwa ambaye alifuatana na Waziri
wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa wamefanya Mkutano wa
Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam ambapo wamezungumzia mapendekezo
yaliyowasilishwa serikalini na Mtoa Huduma za Mawasiliano.
Prof.Makame Mbarawa - Waziri wa Mawasiliano sayansi na Teknolojia Tanzania. |
Hatua ya Serikali kuamua kukata kodi ya shilingi elfu moja
kwenye 'Sim Card' imeibua manung'uniko makubwa kutoka kwa wadau wa mawasiliano
hapa nchini ambapo wamedai kodi hiyo ni mzigo mzito kwa wananchi wa kawaida.
0 comments:
Post a Comment