Image
Image

NANENANE KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI KUYAPIKU MAONESHO YA KITAIFA DODOMA.


Mabanda ya wanyama yakiendelea kutengenezwa
Katika kuhakikisha Maonesho ya Mwaka huu ya siku ya Wakulima Nane Nane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini  yatakayofanyika Mkoani Mbeya yanafana kuliko sehemu nyingine wadau mbali mbali wajitokeza kuyapamba.
 
Hali hiyo inatokana na Maonesho hayo kupelekwa Mkoani Dodoma kitaifa kwa Mwaka wa Sita mfululizo hivyo kuwafanya wakazi wa Nyanda zsa Juu kusini kuonekana kama wamesusiwa hivyo juhudi za maksudi zinafanyika ili kuyanogesha kuzidi ya kitaifa.
 
Baadhi ya Makampuni yaliyojitokeza na kujidhatiti kuyapamba maonesho hayo ni pamoja na Kampuni ya Vinywaji baridi ya SBC (T) LTD  kupitia vinywaji vyao vya Pepsi na Mountain Dew ambao ndiyo wadhamini wakuu wa  Maonesho hayo kwa mwaka huu.
Kampuni nyingine iliyojitokeza ni MLM International Vision (T) LTD ya jijini Mbeya ambayo Mwaka huu imedhamiria kuleta wanyama hai kwa lengo la kukuza utalii wa Ndani ya nchi na kuwasaidia Wananchi ambao hawana fursa za kutembelea mbuga za Wanyama na Vivutio vya Nchini Tanzania.
 
Akizungumzia mikakati ya Kampuni hiyo, Afisa Uhusiano wa MLM, Venance Matinya, amesema Wanyama watakaoletwa ni pamoja na Simba Jike, Simba Dume, Mbega, Chui na Chatu ambao watu mbali mbali watapata fursa za kujua historia zao pamoja na mafunzo  mbali mbali kutoka kwa wataalamu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
 
Matinya ameongeza kuwa Wanyama hao watatumika kama mabalozi wa kutangaza utalii wa ndani na Mijini, ambapo pia ndani ya mabanda ya Wanyama kutakuwa na shughuli mbali mbali hivyo wajasiliamali wanakaribishwa kuuza bidhaa ndogo ndogo.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, William Mkandawile, amesema wahusika wa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na makampuni yanayojihusisha na utalii kuzisaidia sehemu husika kutangaza ili wananchi wapende kutembelea vivutio vilivyokaribu nao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment