Njiwa akiwa amedhoofu kwa Baridi akiwa katika choo cha wanaume |
Mashuhuda wakitoka eneo la tukio |
WAFANYAKAZI
wa Mamlaka ya Reli, kati ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jana walijikuta katika
wakati mgumu na baadhi yao kulazimika kuzikimbia ofisi zao, baada ya ndege aina
ya njiwa kukutuwa katika moja ya choo cha ofisi hiyo akiwa amefungwa hirizi
shingoni, huku akiwa na barua yenye ujumbe wa onyo kali.
Tukio
hilo la aina yake, lilitokea juzi saa mbili asubuhi katika ofisi za mamlaka
hiyo zilizopo eneo la Iyunga Mkoani hapa, hali ambayo mbali na baadhi ya
wafanyakazi wake kuzikimbia ofisi, ilisababisha kuibuka kwa mjadala mkubwa
dhidi ya tukio hilo.
Mwandishi
wetu alifanikiwa kushudia njiwa huyo mweusi akiwa nyuma ya choo cha
kiume katika eneo hilo la ofisi ya mwajiri, huku akiwa amefungwa hirizi
shingoni iliyozungushiwa shanga mchanganyiko wa rangi tatu, ambazo ni Nyekundu,
Njano na Nyeupe.
Mbali
ya kuwa na hirizi hiyo, pia njiwa huyo alikuwa amebeba barua inayodaiwa kuwa ni
ya mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka hiyo (jina limehifadhiwa kwa sababu maalumu)
ambaye anadaiwa hivi karibuni kufukuzwa kazi kwa makosa ya ubadhirifu.
Barua
hiyo ilikuwa na maandishi mekundu yenye ujumbe ulioandikwa kwa lugha mbili za
Kiswahili na kiarabu, ambapo katika maandishi ya Kiswahili yalisomeka “ Naomba
majibu haraka kama mtarudisha binti huyu kazini” ilisema sehemu ya ujumbe huo,
huku ikiwa na orodha ya majina matatu ya viongozi wa shirika hilo.
Mbali
na ujumbe huo ukiwa umeandikwa kwa maandishi ya mkono yaliyokolezwa kwa wino
mwekundu upande wa nyuma, lakini upande wa mbele kulikuwa na maandishi yakiwa
ni barua ya kutaarifiwa kufukuzwa kazi kwa mfanyakazi huyo.
Akizungumzia
tukio hilo, Mwajiri wa mamlaka hiyo kanda ya Mbeya, aliyejitambulisha kwa jina
la Mchaba Mgweno, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba waliobaini ni
wahudumu wa usafi.
Aliongeza kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo aliwaarifu na wafanyakazi wenzake ambao walikusanyika na kumshuhudia Njiwa huyo mweusi akiwa amedhoofika huku akiwa na barua hiyo yenye vitisho.
Alisema
baada ya kushuhudia hali hiyo waliamua kutoa taarifa kituo cha polisi kilichopo
ndani ya shirika hilo, ambapo waliichukua barua hiyo na baadhi ya wafanyakazi
hao wakienda kutoa maelezo kituoni hapo.
“Kwa
kweli hali hii si ya kawaida, ila kwa sasa siwezizungumzia chochote kwa kuwa
hata mimi tukio hili limeniweka katika wakati mgumu na nimeshindwa kuendelea na
majukumu yangu ” alisema Mgweno.
Hata
hivyo kuliibuka malumbano makali kati ya wafanyakazi wa shirika hilo
walioshuhudia tukio hilo, ambapo baadhi yao wakidai kuwa tukio hilo ni la
kutengenezwa kwa lengo la kuchafuana.
“Hebu
angalia hiyo barua yenyewe mbona ni kivuli (Photocopy), kama ingekuwa ni ya
..…. wanamtaja mfanyakazi aliyefukuzwa jina limehifadhiwa ingekuwa ni nakala
halisi, haiwezekani mambo haya ni kutaka kuchafuana tu” alisema mmoja wa wafanyakazi
hao.
Lakini baadhi yao wakiamini kweli kuwa barua hiyo ilitumwa ili itoe vitisho kwa viongozi wa shirika hilo.
Baadhi
ya askari polisi wa kituo cha Tazara walikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanaendelea
na uchunguzi ili kubaini ukweli wake.
“Ndugu
zangu nyie mnajua taratibu za utoaji wa taarifa kwa jeshi hili, maana wapo
wahusika, lakini kwa kifupi sisi tulipokea taarifa na tunaendelea kuzifanyia
kazi” alisema mmoja wa askari hao.
Hata
hivyo, hadi mwandishi wetu anapoondoka eneo la tukio majira ya saa sita mchana
Njiwa huyo alikuwa bado yupo eneo la tukio.
Chanzo mbeya yetu.
0 comments:
Post a Comment