Image
Image

SHULE ZA SEKONDARI ZA KOSA WANAFUNZI KIDATO CHA TANO


Dar es Salaam. 
Hatimaye, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imetoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia kidato cha tano katika sekondari za Serikali na vyuo vya ufundi.
Katika uchaguzi huo, wanafunzi 34,213 kati ya 34,599 waliofaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na Taasisi ya Menejimenti ya Maendeleo ya Maji.
Uteuzi wa wanafunzi hao ambao wanapaswa kuripoti shuleni Julai 29, mwaka huu unamaanisha kwamba kutakuwa na upungufu wa wanafunzi wapatao 10,074 katika shule na vyuo hivyo vya ufundi ambavyo vina uwezo wa kuchukua wanafunzi 43,757.
Upungufu huo unatarajiwa kuwa mkubwa zaidi hasa ikizingatiwa kwamba baadhi ya wanafunzi hao watajiunga na shule za sekondari za binafsi.
Naibu waziri na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo
Aidha, kwa mujibu wa matokeo hayo, ni wanafunzi 386 tu waliofaulu katika madaraja hayo ya kwanza mpaka tatu ambao hawakuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano au vyuo vya ufundi. Hao, wanaweza kujiunga na vyuo vya ualimu.
Kwa mujibu wa Kitabu cha Takwimu cha Wizara ya Elimu (Best), mwaka 2012 wanafunzi 17,095 walichaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali vya ualimu nchini.
Kutokana na takwimu hizo, Serikali italazimika kuchukua wanafunzi wengi zaidi waliopata daraja la nne kujiunga na vyuo vya ualimu kujaza pengo hilo.
Wanafunzi waliopata daraja la nne kwenye mtihani wa kidato cha nne mwaka jana ni 124,260.
Mulugo alisema kuwa wanafunzi waliopata daraja la nne pointi 27 watachaguliwa kujiunga na vyuo vya ualimu endapo wataomba.
“Vigezo vya kujiunga na kidato cha tano na vile vya vyuo vya ualimu ni tofauti, kidato cha tano mwisho anatakiwa mtu mwenye pointi 25 na combination yake (uwiano wa masomo) iwe sawa, ualimu ni pointi 27 wanafunzi wanaomba.
“Mwanzoni walikuwa wanakwenda wenye pointi 28 lakini mwaka jana tukasema hapana iwe pointi 27 na tutachukua kuanzia waliomaliza mwaka 2008 kama wataomba, kwa sasa hivi watu wanaendelea kuwachagua,” alisema Mulugo.
Chanzo Mwananchi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment