Dar es Salaam.
Mfanyabiashara maarufu nchini, Alex Massawe ambaye alikuwa anatafutwa na Polisi
wa Tanzania kwa muda mrefu, amekatwa Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).
Mkuu wa la Shirika la
Polisi la Kimataifa (Interpol), Tawi la Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi
(ACP), Gustav Babile aliliambia gazeti hili jana kwamba Massawe alikamatwa kati
ya Juni 20 na 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai
akitokea Afrika Kusini.
![]() |
| Alex Massawe Akiwa anaonekana hapo ingawa Picha si nzuri sana. |
Babile alisema hivi sasa
walikuwa wanaandaa taratibu za kumrudisha nchini ambako amekuwa akisakwa kwa
muda mrefu.
“Ombi la kuleta mhalifu
nchini kutoka nje ya nchi (extradition request), lina hatua ndefu. Unajua kuna
mlolongo wa taratibu za kutekeleza ili Massawe aletwe. Kwanza lazima Polisi wa
Tanzania watoe tangazo kwa Interpol kuhusu kumsaka mtu huyo ili aletwe,”
alisema Babile.
Alisema Massawe alikamatwa
wakati akifanya taratibu za ukaguzi baada ya kuwasili UAE.
Habari zilizofikia gazeti
hili mapema kutoka Dubai zilieleza kuwa Massawe alikamatwa na maofisa wa
usalama wa UAE kutokana na alama zake za vidole na kuonyesha kuwa alikuwamo
kwenye orodha ya watu waliokuwa wanasakwa na Interpol.
Massawe ambaye anamiliki
majumba na biashara ya utalii katika Miji ya Arusha, Dar es Salaam na Moshi,
inadaiwa kwamba alikutwa na pasi tatu bandia za kusafiria zilizokuwa na majina
tofauti wakati alama zake za vidole zilionyesha anaitwa Alex Massawe.
“Maofisa wa Usalama wa
uwanja wa ndege walimuuliza kuwa wewe ndiye Alex Massawe? Alikana lakini
alielezwa kuwa alama za vidole vinaonyesha anaitwa hivyo,” kilidokeza chanzo
cha habari hizi kwa simu kutoka Dubai. Hata hivyo, Babile alisema hakuwa na
taarifa za Massawe kukutwa na pasi bandia za kusafiria.
Uvumi wa Aprili
Mapema Aprili 27, mwaka huu
kulikuwa na habari kwamba Massawe amekamatwa katika mji mmojawapo ulioko katika
Pwani ya Afrika Kusini.
Habari hizo za kukamatwa
kwa Massawe, ambaye pia hufadhili masuala ya kisiasa na michezo, zilisambaa
kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ya Facebook, Twitter na Jamii Forum.
Kulikuwa kuna mkanganyiko wa taarifa huku wengine wakidai alinaswa akiwa ndani
ya boti huko Afrika Kusini, wengine wakidai alikamatwa wakati akijaribu kuingia
Msumbiji akitokea Malawi.
Akizungumzia hilo
Babile alisema huo ulikuwa ni uzushi na baada ya kuzisikia taarifa hizo
walifuatilia katika maeneo aliyohusishwa kukamatwa na kubaini kwamba hapakuwa
na ukweli wo.
Chanzo Mwananchi.


0 comments:
Post a Comment