Image
Image

Siku moja baada ya timu ya soka ya tanzania Taifa Stars kufungwa bao 1-0 dhidi ya Uganda katika mchezo wa kuwania  kufuzu fainali za michuano ya afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) mwakani,baadhi ya wanamichezo na mashabiki,wametoa maoni tofauti juu sababu za timu hiyo kupoteza mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Wakati baadhi ya wanamichezo hao wakidai kwamba  Stars imefungwa mchezo huo baada ya wachezaji na wananchi kukataa tamaa na kupoteza mwelekeo kwa  kuondolewa kwenye michuano ya kuwania kufuzu kwenye kombe la dunia mwakani nchini Brazil,wengine wamedai timu hiyo haikuibuka na ushindi kutokana na kukosa hamasa ya mashabiki na viongozi uwanjani.

Aidha wanamichezo hao wamesema licha ya stars kutocheza chini ya kiwango,matokeo ya mchezo huo si mwisho wa safari kwani  muda bado upo kwa ajili ya kurekebisha dosari zilizojitokeza na kuweza kubadili matokeo kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya The Cranes mjini Kampala Uganda ndani ya wiki mbili zijazo.

Wamependekeza kwamba safu ya ushambuliaji ya Stars iongezewe makali ili iweze kuhimili ushindani na kuipenya ngome ya Uganda na kuweza kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo wa marudiano wa CHAN.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment