Watu 50 na 3
wamenusurika kufariki dunia na wengine Tisa kufariki kusuatia ajali
iliyohusisha Basi la kampuni ya Sumry lililo tumbukia katika kijiji cha
Sitalike wilaya ya Milele mkoani Katavi.
Ajali
hiyo inaelezwa kuwa ilitokea saa sita usiku kuamkia Julai 5, 2013 basi hilo
lilipokuwa likitokea mjini Sumbawanga kuelekea Mpanda mkoani Katavi likiwa na
abiri waliokuwa wametoka Mbeya.
Kaimu Kamanda wa
Polisi mkoani Katavi Emanuely Nnley alisema jana kuwa ajali hiyo ilihusisha
basi aina ya Nissan Diesel lenye namba T909 AZT mali ya kampuni ya Sumry
lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyetajwa kwa jina na Stephano Chimane
maarufu kwa jina la Ntungu
Alisema basi hilo
lilipofika katika daraja hilo lenye kona kali na mteremko, dereva wake
alishindwa kulimudu na kulenga daraja hali iliyosababisha tairi za nyuma
kupanda juu ya ukingo na kutumbukia mtoni ambapo dereva wa basi hilo aliweza
kutoka na kukimbilia kusikojulikana ...
Mkuu wa mkoa wa
Katavi Dr Rajabu Rutengwe alitoa rambi rambi kwa wafiwa wote na kuwapa pole
wahanga wa ajali hiyo mbaya kutokea tangu mkoa huo uanze.
0 comments:
Post a Comment