Kuringe
Mongi, Dodoma
Mwanafunzi
wa chuo cha ufundi stadi (VETA) Dodoma, Taliki Juma, amedaiwa kujilipua na moto
wa petrol na kusababisha watu wanane kujeruhiwa na yeye mwenyewe kupoteza
maisha, kutokana na kinachodaiwa kuwa wivu wa mapenzi.
Akizungumza
na vyombo vya habari mjini Dodoma, Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma,
Kamishna Msaidizi wa Polisi Suzan Kaganda, amesema marehemu ambaye ni
mwanafunzi wa fani ya magari, alisababisha mlipuko huo kwenye salon ya
kutengenezea nywele, maeneo ya Nzuguni mjini Dodoma.
| Chuo Cha UDOM |
Inadaiwa
kuwa siku ya tukio majira ya saa kumi jioni, marehemu Taliki ambaye ana umri wa
miaka 22, aliingia kwenye salon ya Irene John Mapunda akiwa na galoni ya lita
tano za petrol, ambapo alijimwagia mwilini pamoja na chumba alichokuwepo, na
hatimaye kuwasha moto, uliosababisha mlipuko mkubwa.
Hata hivyo mmoja wa majeruhi wa mkasa huo
Shaban Pili mwanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya sekondari
ya City ya mjini Dodoma amelazwa kwenye hospitali ya mkoa wa dodoma.
Aidha majeruhi
wote wa tukio hilo wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma na mwili wa
marehemu Taliki, upo katika chumba cha maiti cha hospitali hiyo, ukisubiri
taratibu za mazishi kutoka kwa ndugu zake.

0 comments:
Post a Comment