Image
Image

WAZIRI MKUU WA TANZANIA MIZENGO PINDA AZIAGIZA HALMASHAURI LUDEWA KUWAPA ELIMU WANANCHI WAKE JUU YA FURSA ZILIZOPO WILAYANI HUMO.



Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, amesema kuwa wawekezaji wapo hatua za mwisho kuanzisha uzalishaji wa chuma na umeme katika eneo la Ludewa. 

Kufuatia kuanza kwa miradi hiyo, Pinda aliagiza Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kuandaa wananchi kwa kutoa elimu kuhusu fursa, zilizopo za kazi katika eneo hilo. 


Alisema kazi ya Serikali hivi sasa ni kuhakikisha inajenga barabara kupitisha mitambo inayotakiwa kwenye miradi hiyo na kwamba, tayari Sh7 bilioni za awali zimetengwa kwa upanuzi wa barabara.

Kuhusu ujenzi wa barabara ya lami kutoka Itoni, Ludewa hadi Manda, Waziri Pinda alisema tayari Serikali imetenga fedha za upembuzi yakinifu, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi kuhusu miundo mbinu. 

Akizungumzia sekta ya kilimo, Pinda alisema jembe la mkono haliwezi kumaliza matatizo ya mkulima, na kinachotakiwa ni kuangalia uwezekano wa kuwakopesha wakulima matrekta ya bei nafuu. 

Serikali katika eneo hilo inapania kuanza kuzalisha Megawati za umeme 600.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment