Image
Image

NUNDU AWATAKA WAKAZI WA TANGA KUSIKILIZA KILIO CHA WAWEKEZAJI MKOANI HUMO.



 Mbunge wa jimbo la Tanga, Omar Nundu akisikiliza maelekezo kutoka kwa Joseph Mhando mtaalamu wa kusafisha maji yatokayo katika kiwanda cha kutengenezea kanga cha Afritex cha Mkoani Tanga ambaye ana dhamana ya kuhakikisha hayana madhara kwa binadamu na wanyama,Kulia ni Meneja wa kiwanda hicho P.V Kahur.

Mbunge wa Tanga Omar Nundu, anasema kuna haja ya wakazi wa Tanga kusikiza kero zinazowakumba wawekezaji mjini humo.


Akizungumza wakati wa ziara katika viwanda viwili vya nguo mjini humo, alisema viongozi na wananchi wanatakiwa kukaa na wenye viwanda kusikiliza kero zao ili kuimarisha shuguli za kila mmoja kiuchumi.

Alisema lengo ni kuangalia jinsi ya kutatua kero hizo, kutokana na viwanda vingi kusimamisha uzalishaji. 

Aidha Nundu aliongeza kwa kusema viwanda vilivyokufa vinatakiwa kufufuliwa, vile vinavyofanya kazi viungwe mkono na wananchi kupenda bidhaa zake kutoruhusu bidhaa za nje kuhodhi soko. 

Hata hivyo ameongeza kwa kusema kwamba  Tanga ina fursa ya kuwa na viwanda na kuwavutia wawekezaji kutokana na miundo mbinu ya bandari na reli.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment