Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama
ya Kimataifa ya Jinai ICC, Bi. Fatou Bensouda, ameondoa mashahidi watatu kwenye
kesi ya jinai dhidi ya binadamu inayomkabili Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Bensouda amesema mashahidi wawili wamesisitiza kwamba hawawezi kuendelea kuwa
mashahidi kwenye kesi hiyo kutokana na kuhofia usalama wao.
Amesema pia kuwa,
ametathmini ushahidi wa shahidi mwengine na ameona hauna umuhimu mkubwa na kwa
mantiki hiyo ameamua kumuondoa.
Itakumbukwa kuwa mahakama hiyo ya ICC majuma
kadhaa yaliyopita iliamua kwamba, Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto
atahudhuria tu vikao muhimu vya kesi yake mjini Hague na kisha kushiriki kwenye
vikao vya kawaida kwa njia ya video.
Wachambuzi wa masuala ya kisheria wanasema
hatua hiyo ina maana kwamba kesi dhidi ya Rais Kenyatta na Makamu wake
zinaendelea kuwa dhaifu na huenda wakafutiwa mashtaka iwapo matukio kama hayo
yataendelea kushuhudiwa.
0 comments:
Post a Comment