Askari wa utawala haramu wa Kizayuni, wamewashambulia mateka wa
Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela ya kuogofya ya utawala huo ya Eshal.
Shambulizi hilo lilifanyika jana usiku na kuwajeruhi mateka kadhaa wa
Kipalestina wanaoshikiliwa kinyume cha sheria katika jela hiyo ya kutisha.
Waziri anayeshughulikia masuala ya mateka wa Kipalestina katika jela za Israel
Issa Qaraqe amelaani vikali shambulizi hilo la askari wa utawala huo katili wa
Kizayuni dhidi ya mateka hao wa Kipalestina na kuitaka jamii ya kimataifa
kuushinikiza utawala huo kuwaachia huru mateka hao.
Kuachiliwa huru mateka wa
Kipalestina kutoka katika jela za kutisha za utawala haramu wa Kizayuni, ni
moja ya masharti ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina kwa ajili ya kuanza tena
mazungumzo na utawala wa Kizayuni.
Inatazamiwa kuwa, leo Mamlaka ya Ndani ya
Palestina itatoa jibu kuhusiana na pendekezo la John Kerry, Waziri wa Mambo ya
Nje ya Marekani juu ya kuanza tena mazungumzo kati ya utawala wa Kizayuni wa
Israel na mamlaka hiyo.
Makundi ya muqawama ya Palestina, yanaamini kuwa,
mazungumzo hayo hayana faida yoyote kwa raia wa Palestina.
0 comments:
Post a Comment