Zimbabwe imefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Cosafa baada ya
kufanikiwa kuwachapa Malawi kwa mikwaju ya penati baada ya kwenda sare ya bao
1-1 katika muda wa kawaida wa mchezo wao wa hatua ya robo fainali katika mchezo
uliofanyika hii leo huko Kitwe nchini Zambia.
Ocean
Mushure alifunga penato ya ushindi kwa washindi hao mara nne wa michuano hiyo.
Katika
muda wa kawaida Zimbabwe walikuwa wa kwanza kushambulia na kuandika bao
la uongozi kwa mpira wa kurudi uliofungwa na Masimba Mambare kunako dakika ya.
Mshambuliaji
wa Malawi James Sangala alitolewa nje yaw a uwanja baada ya kupewa kadi ya pili
ya njano kabla ya mapumziko kitendap ambacho kiliivuruga the Flames.
Lakini hata hivyo kunako dakika ya 85 ya mchezo , Boniface Kaulesi
alifanikiwa kuandika bao la kuswazisha na mchezo kuelekea katika dakika za
nyongeza na hatimaye kufikia katika hatua ya mikwaju ya penati.
Katika
hatua nyingine Afrika ya kusini nao wamefanikiwa kutinga katika hatua hiyo ya
nusu fainali baada ya kuwachapa Namibia kwa bao 2-1 mchezo ambao pia umepigwa
hii leo.
Bafana
Bafana walikuwa wakicheza mechi yao kwanza ya michuano hiyo kufuatia kupata
nafasi ya kuingia moja kwa moja katika michuano hiyo.
Mchezaji
alieingia kutoka benchi Shongwe Jabulani aliandika bao kwanza kwa mpira mrefu
muda mfupi baada ya kuanza kipindi cha pili.
Afrika
kusini pia wakafanikiwa kuandika bao la pili kupitia kwa Kekana Hlompho akiwa
katika kona ya kisanduku cha hatari.
Namibia
walifanikiwa kupata penati kufuatia Mkhwanazi Buhlke kuunawa mpira ndani ya
kisanduku cha 18 lakini hata hivyoWilly Stephanus alishindwa kuandika bao kwa pigo la kwanza kabla ya
mwamuzi kumtaka kurudia penati yake ambapo kiungo huyo aliiukwamisha mpira
kambani.



0 comments:
Post a Comment