Polisi wa Wilaya ya Hai
wakianda mwili wa mfanyabiashara wa madini Erasito Msuya aliyeuawa kwa kupigwa
risasi katika eneo la Wasomali, mkoani Kilimanjaro, kwa ajili ya kuupeleka
chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospiotali ya wilaya hiyo.
MFANYABIASHARA tajiri wa Mirerani na Jijini Arusha, Erasto
Msuya, ameuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 kwa kutumia bunduki aina ya Sub
Machine Gun (SMG), jana mchana mjini Moshi.
Erasto anayemiliki vitega uchumi kadhaa na anayeaminika kuwa
miongoni mwa wafanyabiashara wa Mirerani wanaoongoza kwa utajiri,aliuawa jana saa 7:00 mchana wilayani Hai mkoani
Kilimanjaro
.
“Eneo la tukio kumeokotwa maganda karibu 21 ya risasi
zinazoaminika ni za SMG, yaani mwili ni matobo kila sehemu kwa kweli ameuawa
kinyama sana,” alisema polisi mmoja wa Kituo cha Bomang’ombe.
Kufuatia mauaji hayo yaliyotokea kati ya neo la Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na mji wa Bomang’ombe, mji huo
ulifurika magari ya wachimbaji kutoka Moshi, Arusha na Mererani.
Habari za uhakika zilieleza kuwa wauaji wake walikuwa katika
pikipiki na baada ya kumminia risasi hizo, walimpora kibegi ambacho
haikujulikana kama kilikuwa na madini ama mamilioni ya fedha.
Kulingana na vyanzo vya habari, mfanyabiashara huyo
alipigiwa simu na kukubaliana kukutana katikati ya mji wa Bomang’ombe na
makutano ya Barabara ya Kia katika Barabara Kuu ya Hai kwenda Arusha.
RPC Kilimanjaro afafanua alivyouawa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema
kuwa mfanyabiashara huyo aliuawa saa 7:00 mchana eneo la Mjohoroni kati ya mji
wa Bomang’ombe na makutano ya barabara ya Kia.
“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Eransto alikuwa akitokea
Moshi kuelekea Arusha, na alipofika hilo eneo la Mjohoroni alichepuka na kwenda
meta 300 nje ya barabara,” alisema.
Kamanda Boaz alisema alipofika eneo hilo, alikutana na
vijana wawili waliokuwa na pikipiki ambao waliingia ndani ya gari kwa lengo la
kufanya mazungumzo yanayodhaniwa ni ya kibiashara.
Hata hivyo, muda mfupi tu Erasto alishuka kwenye gari lake
na kuanza kukimbia na ndipo mmoja kati ya wale vijana alishuka kwenye gari la
Erasto na kuanza kumminia risasi nyingi. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment