Raia wa Bulgaria akiwa chini ya Ulinzi baada ya
kupata kichapo kwa kudaiwa kuiba fedha kwenye mashine ya kutolea fedha (ATM) ya
BOA tawi la Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam jana.
DAR ES SAALM.
MSAKO wa wezi wa kwenye Mashine za Kutolea Fedha (ATM), umeanza kuzaa matunda baada ya raia wa Bulgaria kukamatwa akiiba kwenye ATM ya Bank of Africa (BOA), Tawi la Afrikana, Kinondoni, Dar es Salaam.
MSAKO wa wezi wa kwenye Mashine za Kutolea Fedha (ATM), umeanza kuzaa matunda baada ya raia wa Bulgaria kukamatwa akiiba kwenye ATM ya Bank of Africa (BOA), Tawi la Afrikana, Kinondoni, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa za benki, mtuhumiwa huyo ambaye
hakutajwa jina lake alikamatwa baada ya kamera maalumu zilizowekwa kwenye ATM
za BOA, kumtambua kuwa ni mwizi sugu wa benki hiyo anayetafutwa.
Mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo ambaye hakupenda kutajwa
jina kwa kuwa si msemaji, alisema tukio hilo lilitokea jana saa 12 asubuhi
baada ya mtuhumiwa huyo kuwekewa mitambo maalumu ya kumnasa.
Alisema benki hiyo ilipelekewa malalamiko na baadhi ya
wateja kwamba wakienda kutoa fedha kwenye ATM wan
akuta akaunti zao hazina salio wakati wanaamini zilikuwa na fedha.
akuta akaunti zao hazina salio wakati wanaamini zilikuwa na fedha.
Chanzo hicho cha habari kilidai kuwa baada ya kupelekewa
malalamiko hayo, waliweka mitambo maalumu ya kuwawezesha walinzi wa maeneo ya
ATM za BOA kumbaini mtu atakayetoa fedha kwa njia ya wizi.
“Kama Benki tuliweka mtambo maalumu na mtuhumiwa huyo
alionekana kwenye mtambo wetu, hivyo tuliwaagiza walinzi wetu watakapomwona mtu
huyo wamkamate haraka sana,”alisema.
Alisema mtuhumiwa huyo alianza mchezo huo kwa muda mrefu
ambapo kwa kutumia kadi za ATM zisizojulikana idadi yake, alikuwa anakwenda
kwenye ATM mbalimbali za benki hiyo na kutoa fedha hadi Sh10 milioni.
Kuhusu tukio la jana, mmoja wa walinzi wa BOA
aliyejitambulisha kwa jina moja la Frenky alisema mtuhumiwa huyo alipofika
kwenye ATM hiyo aliingia na kuchukua fedha ambazo alizipeleka kwenye gari lake.
Frenky alisema baada ya kupeleka fedha hizo, alirudi kwa mara ya pili ili
achukue fedha nyingine ndipo walinzi hao walimkamata na kumfunga pingu.
“Huyu mtuhumiwa mwenye asili ya Kiarabu alifika na gari lake
saa 12 asubuhi, aliingia kwenye ATM na kutoa fedha ambazo hazikujulikana ni
shilingi ngapi na kuzipeleka kwenye gari lake, baadaye alirejea tena kwa ajili
ya kutoa fedha zingine, wakati anaingia ndipo alipokamatwa na mlinzi aliyekuwa
analinda hapo,” alisema Frenky.
Kamanda wa Polisi Kinondoni, Camilius Wambura alikiri
kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi hilo huku
uchunguzi dhidi yake ukiendelea.
“Ni kweli taarifa nimezipata, mtuhumiwa amekamatwa, bado
hatujajua ni kiasi gani ambacho ameiba kwa kutumia mtandao, tunaendelea na
uchunguzi,” alisema Wambura.
Tukio kama hili lilishawahi kutokea mkoani Mwanza Februari
19 mwaka huu na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na maofisa ya
Benki ya NMB liliwatia mbaroni watu watatu ambao walidaiwa kuiba kiasi cha
Sh700 milioni kwa nyakati tofauti. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment