Mbunge wa Jimbo la Segerea, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akiwaonyesha baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilala (Jimbo la Segerea), kituo kipya cha Polisi cha Tabata, Dar es Salaam, walipokuwa kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu jimboni hapo.
Dk. Makongoro Mahanga na Diwani wa Kata ya Tabata, Mtumwa Mohamed pamoja na wajumbe wakikagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne akatika Shule ya Msingi Tabata jijini Dar es salaam.
Dk. Mahanga akitoa maagizo kwa watendaji wa Kata ya Kimanga, kuhakikisha kwamba wanabomoa haraka iwezekanavyo msingi wa bendera ya CHADEMA, uliojengwa kwenye eneo la Stendi ya Dcaladala ya Kimanga inayotarajiwa kufanyiwa matengenezo wiki hii.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Ilala, wakikagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kinyerezi- Segerea.
Mhandisi wa Manispaa ya Ilala, Muhinda Kassim akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa miradi.
Mkazi wa Kinyerezi akitoa ushauri kwa wahandisi wa Tanroads Dcar es Salaam kuhakikisha wanatunza vizuri barabara ikiwemo kuwela alama.
Mmoja wa wahandisi wa Tanroads akielezea kuhusu maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kinyerezi-Segerea.
Dk. Mahanga akizungumza na wahandisi wa Tanroad Mkoa wa Dar es Salaam.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilala, wakikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Tabata-Liwiti.
0 comments:
Post a Comment