Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Ahmed Kipozi akiangalia magonjwa ya mifugo kupitia darubini wakati alipotembelea banda la halamshauri ya Mkinga mkoa wa Tanga kitendo cha mifugo katika maonyesho ya wakulima ya nanenane kanda ya mashiriki katika viwanja vya kimataifa vya Mwl Julius Nyerere mkoani Morogoro. kushoto ni Dk Benedetti Gunza.
MAONYESHO ya wakulima nanenane kanda ya mashariki yanaonekana kudorora kutokana na idadi ndogo ya wananchi wanaohudhuria katika maonyesho hayo na baadhi ya wizara kuwa na madeni yaliyochangia malengo kutofikiwa.
Mwenyekiti wa chama cha wakulima kanda ya mashariki TASO Mohamed Mzee akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya nanenane alisema kuwa maonyesho ya mwaka huu yamekuwa si ya kuridhisha kutokana na kuwepo kwa idadi ndogo ya watu wanaojitokeza katika viwanja hivyo.
Aidha alizitaja wizara za Kilimo,chakula na Ushirika,Viwanda na biashara pamoja na wizara ya Mifugo na uvuvi zimechangia kwa kiasi kikubwa kutopfikiwa kwa malengo yaliyokuwa yamewekwa na TASO.
Mzee alisema wizara hizo zinadaiwa zaidi ya shilingi 56 milioni na kwamba hiyo imechangia kukwamisha baadhi ya malengo ambayo kamati ilikuwa imejiwekea.
Mwenyekiti huyo alisema malengo ya TASO kwa mwaka huu ilidhamilia kuweka rami katika barabara zake ili kupunguza vumbi , kuongeza mabomba ya maji, taa katika barabara mablimbali sambamba na kumaliza kujenga ukuta katika sehemu ambayo haina ukuta na kwamba zoezi hilo limekwama kutokana na madeni hayo.
Pia Mzee alisema hadi sasa TASO inadai kiasi cha shilingi 250 milioni kutoka bodi mbalimbali, halmashauri pamoja na taasisi huku zikiwa zimebaki siku chache kumalizika kwa maonyesho hayo na kuongeza kuwa madeni haya yamekuwa sugu.
Alisema kuwa pamoja na changamoto hizo lakini TASO imejitahidi kuhakikisha maonyesho hayo yanakuwa na mvuto kwa ikiwa ni kuongeza wateja wapya wanaonyesha bidhaa zao ili watazamaji waweze kujifunza na kubadilisha uzoefu.
Mwandishi waa habari hizi alishuhudia idadi ndogo ya wananchi wanaoingia katika maonyesho hayo,ambapo baadhi ya wananchi walisema kuwa nanenane ya mwaka huu haina msisimuko kutokana na uhamasishaji kuwa mdogo.
Wananchi hao walisema kuwa chanzo kikubwa cha kudorora kwa maonyesho hayo ni kwa miaka minne mfululizo maonyesho hayo kitaifa yamekuwa yakifanyika kanda ya kati bila kubadilika.
0 comments:
Post a Comment