Kama kweli tunataka
kuliokota taifa na janga la ajali za pikipiki ni lazima waendesha pikipiki
waheshimu utawala wa sheria. Dereva kama hana mafunzo ya udereva au leseni,
asiruhusiwe kuendesha chombo cha moto.
Huu ndio usafiri wetu
wa haraka dar lakini kwa mikoa mingine haya ndio magari, piki piki hizi
nimevutiwa nazo leo hii katika kituo uchwara Tabata kinyerezi zikiwa zimepaki
kwa kusubiria abiria.
Huu ndio usafiri wetu wa haraka dar lakini kwa mikoa mingine haya ndio magari, piki piki hizi nimevutiwa nazo leo hii katika kituo uchwara Tabata kinyerezi zikiwa zimepaki kwa kusubiria abiria.
TANGU Serikali ya Tanzania iridhie pikipiki maarufu kama
bodaboda kubeba abiria, tumeshuhudia ndugu na marafiki zetu wakipoteza maisha
na hakuna ubishi sasa ni janga la kitaifa.
Inavyoonekana, wakati Serikali
ikiruhusu pikipiki kubeba abiria ilikuwa haijajiandaa kikamilifu na badala yake
ilijikita kuangalia mapato ya kodi yatakayotokana na biashara ya kubeba abiria
na kikubwa zaidi kutengeneza ajira kwa vijana.
Naamini Serikali haikujiandaa
kwa sababu leo hii si ajabu kijana kujifunza pikipiki kwa dakika 30 na kuingia
barabarani kubeba abiria.
Serikali iko kimya!.
Takwimu zinatuonyesha tangu 2009
serikali ilipokubali pikipiki kubeba abiria mpaka mwaka jana, pikipiki 330,882
zimesajiliwa nchini sawa na asilimia 60 ya usafiri huo.
Ongezeko hilo la
pikipiki limekuja na janga lingine kwa Watanzania.
Vifo na majeruhi wamekuwa
wakiongezeka siku hadi siku na kuwasababishia baadhi ya vijana na abiria
ulemavu wa kudumu.
Sababu kubwa ya vijana na abiria wa pikipiki kupata ulemavu
wa kudumu ni uzembe wa madereva uchwara kufanya kazi hiyo.
Tunaambiwa mwaka
2011 pekee, kulikuwapo ajali 5,384 za pikipiki zilizosababisha vifo vya watu
945 na majeruhi 5,506, wakati mwaka 2010 kuliwapo ajali 4,463 zilizosababisha
vifo vya watu 683 na majeruhi 4,471.
Takwimu za hivi karibuni kabisa–Januari
mpaka Septemba 2012 kulikuwapo ajali za pikipiki 4,142 zilizosababisha vifo 720
na kuwaacha Watanzania wenzetu 4,057 wakiwa walemavu.
Nimeanza kwa kuweka
takwimu hizo ili ninaposema suala la Bodaboda sasa ni janga la kitaifa,
Watanzania na mamlaka zinazohusika ikiwamo rafiki zangu trafiki waone ukubwa wa
tatizo.
Hakuna ubishi kwamba mamlaka zenye dhamana za kusimamia usafiri huo
zimelala na kusababisha kuwapo kwa walemavu na watu wengi kupoteza maisha.
Si
ajabu kukuta askari wa usalama barabarani wakiwa kazini, lakini vijana
wakiendesha pikipiki bila leseni, na kutovaa kofia ngumu.
Sote tunafahamu,
katikati ya mji tena kwenye msongamano mkubwa tumekuwa tukishuhudia wakiendesha
kwa mwendo mkubwa tena mbele ya askari wa usalama barabarani?.
Tatizo
ninalolioa hapa ni udereva kuchukuliwa kama sio taaluma, Ndio maana leo muuza
urembo anaweza kununua pikipiki, hana leseni, wala hajawahi kuendesha pikipiki
na akaanza kuendesha.
Huu sasa ni wakati wa kujifunza kwa jeshi la polisi na mwisho wa siku kuonekana kana kwamba ni wadhaifu hasa kikosi cha
usalama barabarani kumbe ni watu wachache wanalipotezea sifa jeshi hilo
Sheria ziko wazi kwamba mtu hawezi kuendesha
chombo cha moto bila kuwa na leseni tena aliyoipata kihalali, lakini wapo
bodaboda wanakamatwa leo anahonga, kesho yuko tena barabarani.
Kama kweli
polisi wetu wa usalama barabarani wangekuwa na ratiba za kazi kila siku kwamba
leo tushughulike na bodaboda wasio na leseni, hakika tungepunguza ajali za
pikipiki.
Si ajabu leo ukamuona mwendesha bodaboda akilipita (overtake) gari
kupitia upande wa kushoto, anaonyesha taa akimaanisha anakata kulia, lakini
anakata kushoto.
Dereva kama
hana mafunzo ya udereva au leseni, asiruhusiwe kuendesha chombo cha moto.
Tusihalalishe
uvunjifu wa sheria kwani tutawapoteza vijana wengi kwa wanajisikia fahari kubwa
kuendesha pikipiki kwa mwendo kasi bila kujali uhai wao.
Tuwasaidie vijana kwa
kuwa wengi wao hajui wanalolifanya, polisi wa usalama barabarani wawakamate
kuwaadhibu kwa mujibu wa sheria kwani kufanya hivyo ni kwa faida yao na watu
wengine wanaotumia usafiri huo.
Kwa mtazamo wangu polisi wa usalama wa
barabarani wanatakiwa kufanya operesheni maalumu ya kukamata pikipiki zote
abazo zina makosa ya usalama barabarani.
Pili, waendesha bodaboda ambao
watakutwa hawana leseni, hawataruhusiwa kuendesha mpaka waende shule na baada
ya kufuzu waonyeshe cheti na leseni halali ya udereva.
Naamini kama tukiweka
utaratibu huo hakika hakuna atayakeingia barabarani bila kuwa amepata mafunzo
ya udereva na kujua alama za barabarani pamoja na sheria nyingine.
Haiwezekani
leo ni mwaka wa tatu tangu Serikali iruhusu biashara ya Bodaboda bado wapo
wanaoibuka na kuendesha pikipiki bila leseni wala kujua sheria za barabarani.
Trafiki
wanatakiwa kuchukua hatua kali ya kuwadhibiti waendesha pikipiki ambao hawavai
kofia ngumu, walevi, na waendesha pikipiki kwa kasi.
Ni fedheha kwa jeshi la
polisi kuwaachia waendesha pikipiki kuvunja sheria za usalama barabarani.
, Jambo
lingine la kushangaza ni tabia ya waendesha pikipiki kusababisha ajali na kuwa
wa kwanza kupigiana simu na kuharibu gari na wakati mwingine kuwajerihi gari
ambalo limegongwa na dereva wa bodaboda.
Ni jambo la kushangaza! Kwanini,
polisi wa usalama barabarani wametoa uhuru mkubwa kwa waendesha pikipiki?
Wanachukua sheria mkononi na hakuna anayewauliza.
Nadhubutu kusema pengine
wanakula rushwa ya Sh2,000 hadi 10,000 kutoka kwa baadhi madereva wa boda boda.
Kutokana
na hali hiyo kama polisi wasipojipanga upya kwa ajili ya kuwadhibiti waendesha
bodaboda, usafiri huo utaendela kuwaua watu wengi.
Trafiki wetu watambue
kwamba hakuna mahali mtu anaweza kununua uhai.
Pia madereva bodaboda na abiria
wajue hakuna duka la kununua uhai.
Kila mmoja awajibike kwa mujibu wa sheria
kulinda uhai wa mwenzie.
0 comments:
Post a Comment