Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa
Kampuni ya kichina ya CPTDC iliyopewa tenda ya kutandaza mabomba ya gesi kutoka
Mtwara hadi Dar es Salaam, alipokuwa katika ziara ya siku moja ya kukagua
utekelezaji wa maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi, juzi eneo la
Somanga Fungu, wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi.
Sehemu ya mabomba ya gesi yakiwa eneo la kuhifadhia la Nyamwage,
Rufiji.Profesa Muhongo akiangalia kipenyo cha bomba ambacho ni mita moja.
Profesa Muhongo akioneshwa sehemu
ya bomba itakayounganishwa na bomba linguine.
Watalaamu wa ubora wa ufungaji mabomba ya gesi kutoka
Afrika Kusini wakimueleza Waziri Muhongo kuhusu umakini wakati wa kuunganisha
mabomba hayo.
Profesa Muhongo akiwa eneo la kuhifadhia mabaomba, Nyamwage,
wilayani Rufiji. Mabomba hayo yalianza kuunganishwa jana.
Waziri Muhongo akiwa katika picha
ya pamoja na wafanyakazi wa kamapuni hiyo ya kichina.
Waandishi wa habari walioambatana na Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo (amezibwa), wakiangalia nyaya za mkongo
zitakazotandazwa sambamba na mabomba ya gesi kwa ajili ya usalama, zilizokuwa
kwenye lori katika ghala la kampuni hiyo ya kichina wilayani Mkuranga, Pwani.
Baadhi ya mitambo ikiwa imefungwa
wilayani Mkuranga, Pwani, kwa ajili ya kuongezea unene wa mabomba maalumu ya
gesi yatakayotandazwa baharini.
0 comments:
Post a Comment