Umoja wa
Mataifa umesema kuwa mwanajeshi wake mmoja wa kutunza amani ameuawa na wengine
watatu kujeruhiwa kufuatia mapigano makali kati ya na wapiganaji wa waasi
Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Msemaji wa Umoja wa
Mataifa mjini New York, Farhan Haq, hata hivyo hajatangaza uraia wa wanajeshi
waliouawa au kujeruhiwa.
Wanajeshi hao wa Umoja
wa Mataifa walitumia ndege za helicopta kuwasukuma nyuma wapiganaji wa M23
karibu na mji wa Goma, ambao ndio mji mkubwa zaidi katika eneo hilo la Mashariki.
Watu themanini
waliuawa kwenye mapigano hayo wiki iliyopita.
Mwaka wa 2012, waasi
wa M23 waliuteka mji huo kwa muda kabla ya kuondoka kufuatia shinikizo kutoka
kwa jamii ya kimataifa.
Umoja wa Mataifa
Umetuma kikosi maalum katika eneo hilo lenya utajiri mkubwa wa madini
kukabiliana na waasi hao.
Wanajeshi hao wa Umoja
wa Mataifa MONUSCO, wanapambana na wapiganaji hao wa waasi kwa ushirikiano na
wanajeshi wa serikali.
Silaha kali
Jeshi hilo la Monusco
limelazimika kufanya mashambulio ya anga na ardhini ili kuzuia waasi hao wa M23
kukaribia Goma na ripoti zinasema mapigano makali yanaendelea katika maeneo ya
milima ya Kibati, takriban kilomita kumi na tano Kaskazini mwa Goma.
Watu wapatano laki
mbili wanasemekana kuishi katika eneo hilo la Kibati.
Wapiganaji wa M23
wamesema kuwa wanajeshi wa Congo na wenzao wa Umoja wa Mataifa walifanya
mashambulio ya anga na ardhini katika maeneo wanayoyadhibiti, Kaskazini mwa
Goma.
Daktarri mmoja mjini
Goma, Isaac Warwanamiza, ameliambia shirika la habari la AP kuwa aliona miili
ya watu themanini na wawili, ishirini na tatu zikiwa za wanajeshi wa serikali.
Umoja wa Mataifa una zaidi wanajeshi elfu kumi na nane
nchini Congo.
0 comments:
Post a Comment