Mtu
mmoja amefariki dunia na 15 wamejeruhiwa baada ya basi la Kampuni
ya Hood likitokea kilombero kwenda jijini Dar es salaam
kumgonga mtembea kwa miguu na kisha kuacha njia na kupinduka katika eneo
la Kiembeni Mikese Mkoani Morogoro.
Mkuu
wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro Bonifasi Mbao
akizungumza kwenye eneo la tukio amesema chanzo cha ajali hiyo ni
mwendo kasi ambapo dereva wa basi gari ilimshinda na kugonga
mtembea kwa miguu na kisha kupinduka ambapo dereva wa basi amekimbia mara
baada ya tukio la ajali
Taarifa
za madaktari katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro
zimeeleza majeruhi wanaendelea na matibabu na mwili wa marehemu
umehifahiwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa morogoro .
ITV SOURCE.
0 comments:
Post a Comment