Jukwaa la Katiba Tanzania JUKATA,
lililokuwa ni miongoni mwa waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi wa Zimbabwe
uliofanyika hivi karibuni, limesema uchaguzi huo ulikuwa huru na haki
kulinganisha na ule wa mwaka 2008, licha ya changamoto kadhaa zilizojitokeza.
Hayo yamebainishwa na jukwaa hilo
mbele ya waandishi wa habari wakitoa tamko lao kuhusiana na uchaguzi huo lililojikita
zaidi katika mchakato wa kupiga kura ndani ya katiba mpya ya nchi hiyo na
mafunzo muhimu kwa Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya jopo la
waangalizi wa jukwaa hilo waliokuwa nchini humo, mwenyekiti wake Asha Aboud,
amesema kulikuwa na kasoro chache katika suala la kuandikisha wapiga kura
ikiwemo siku chache za kazi hiyo ,ambapo kuhusu kampeni amesema zilienda vizuri
licha ya kuwepo kwa matukio machache ya uvunjifu wa amani.
Jukwaa hilo limezungumzia uzoefu na
mafunzo walioupata kutoka katoka uchaguzi huo wa Zimbabwe, ikiwemo uchaguzi huo
kufanyika siku ya kazi na siku hiyo itangazwe mapumziko ili wananchi wapate
nafasi ya kutimiza haki yao ya msingi.
Aidha wamezungumzia umuhimu wa tume
ya uchaguzi kuaminika kufuatia vyama vya upinzani kutuhumu vitendo vya tume
hiyo kutotoa taarifa muhimu kwa wakati.
0 comments:
Post a Comment