Image
Image

OBASANJO AKIRI KUWA UCHAGUZI WA ZIMBABWE NI WA HURU NA HAKI.





Umoja wa Afrika umesema uchaguzi wa Zimbabwe  ulikuwa  huru na wa  haki lakini  unataka taarifa zaidi kuhusu matatizo yalioripotiwa.

Olusegun Obasanjo ambaye aliongoza timu ya wafuatiliaji wa Umoja wa Afrika , amesema  Ijumaa  kwamba kulikuwa na hitilafu ambazo zingeweza kuepukwa .

Obasanjo amesema timu yake imeona idadi kubwa ya wapiga kura ambao walizuiwa kupiga kura. Lakini akaongeza kuwa  haamini  hali hiyo ilitokea kwingine kuweza kuathiri matokeo ya jumla ya uchaguzi huo.

Chama cha rais wa muda mrefu Robert Mugabe kimedai ushindi katika uchaguzi wa Jumatano  ingawa matokeo ya mwisho bado hayajatangazwa .

Mpinzani wake waziri mkuu Morgan Tsvangirai  jana Alhamis  alisema kulikuwa na wizi wa kura na kwmaba uchaguzi huo huashirii  matakwa halisi ya wananchi wa Zimbabwe
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment