Hamisi Kiiza.
Hatimaye mshambuliaji
wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ amesaini Mkataba wa miaka miwili
kuendelea kuichezea klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam.
Kwa mjibu wa Afisa
habari wa Yanga Baraka Kizuguto amesema Kiiza amesaini mkataba huo wa miaka
miwili usiku wa kuamkia leo ambapo sasa ataendelea kuichezea klabu ya Yanga
hadi mwaka 2015.
Mfumania nyavu huyo
hodari kutoka Uganda awali alishindwa na Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Tanzania
bara kutokana na kutaka kuongezwa dau kubwa la usajili pamoja na mshahara
mnono.
Usajili wa Kiiza
umefikisha idadi ya wachezaji wanne kwa
wachezaji wa kigeni wengine ni beki Mbuyu Twite, kiungo Haruna Niyonzima
wote kutoka Rwanda na mshambuliaji Didier Kavumbangu wa Burundi, ambapo sasa
Yanga wamebakiwa na nafasi moja ya mchezaji wa kigeni huku klabu hiyo
ikiendelea kupigana vikumbo na mahasimu wao wa kubwa Simba juu ya kutaka
kumsajili mshambuliaji wa Uganda Moses Oloya anayesakata kandanda katika klabu
ya Saigon Xuan Thanh ya Vietnamambaye mkataba wake unamalizika Agosti 31 mwaka
huu.
0 comments:
Post a Comment