Mwandishi wa Habari
Juma Abdallah wa Zenji Fm Radio akiuliza suali kwa Mtaalamu wa mbu waenezao
Malaria katika Kitengo cha kudhibiti Malaria Zanzibar (ZMCP) Khamis Ameir
(hayupo pichani) juu ya mikakati ya upigaji dawa huko katika ukumbi wa
kitengo cha kuzibiti Malaria mwanakwerekwe Zanzibar.
Kaimu Meneja wa Kitengo cha kudhibiti
Malaria Zanzibar (ZMCP) Mwinyi Issa Mselem akifafanu kitu juu ya mikakati ya
kumaliza Malaria Zanzibar katika mkutano na Waandishi wa Habari, huko katika
ukumbi wa kitengo cha kuzibiti Malaria mwanakwerekwe Zanzibar.
Mtaalamu wa mbu waenezao Malaria katika
Kitengo cha kudhibiti Malaria Zanzibar (ZMCP) Khamis Ameir, akionyesha moja mbu
waenezao Malaria katika mkutano na Waandishi wa Habari huko katika ukumbi wa
kitengo cha kuzibiti Malaria mwanakwerekwe Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari
waliokuwepo katika ukumbi wa kitengo cha kuzibiti Malaria
mwanakwerekwe Zanzibar, wakifuatilia kwa makini taarifa ya Kaimu Meneja wa
Kitengo cha kuzibiti Malaria Zanzibar (ZMCP) Mwinyi Issa Mselem hayupo pichani.
(Picha
na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar).
0 comments:
Post a Comment