Kituo cha Sheria na Utetezi wa Haki za
Binadamu (LHRC) na Chama Cha Wanasheria Tanzanyika vimefungua kesi ya
Kikatiba katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, vikiomba mahakama hiyo
itoe tafsiri za kisheria katika baadhi ya Ibara.
Kesi hiyo ya Kikatiba ambayo imepewa namba 24
ya mwaka huu, na ambayo bado haijapangiwa jaji, wadaiwa ni Waziri Mkuu Mizengo
Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mizengo Pinda.
Taasisi hizo ambazo zinatetewa na mawakili wa
kujitegemea Harold Sungusia, Francis Stolla na wengine 17, kwa mujibu wa hati
yao ya madai, walalamikaji hao wamewasilisha jumla ya maombi mawili ambayo
wanaomba mahakama itoe tafsiri ya kisheria katika Ibara hizo kwa kuwa
wamewasilisha kesi hiyo ya Kikatiba chini ya sehemu ya Tatu ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo
inaainisha Haki na Wajibu
Muhimu.
•
Wakili Sungusia
alilitaja ombi la kwanza kuwa, wanaiomba mahakama hiyo itamke kuwa ibara ya
100(1) ya Katiba ya nchi inayotoa uhuru wa majadiliano kwa wabunge wawapo
ndani ya bunge ambayo inasomeka hivi:
“kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano
na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo
chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katikaMahakama au mahali penginepo nje
ya Bunge.”
Wakili Sungusia anadai kuwa Ibara hiyo ina
ubaguzi ndani yake kwani inayoa uhuru kwa mbunge kujadili ndani ya bunge na
wakati anajadili jambo hata kama amevunja haki za mtu mwingine hataweza
kushitakiwa wala kuhojiwa jambo ambalo anadai linakinzana na Ibara ya 13(2) ya
Katiba ambapo Ibara hii inasomeka hivi; “ Ni marufuku kwa sheria yoyote
iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti
lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake’.
‘…sisi tunaomba mahakama itamke wazi kuwa Ibara
ya 100(1) inakwenda kinyume na matakwa ya Ibara 13(2).
Zinakinzana, kwa kuwa
ibara ya 100(1) ya Katiba inatoa haki tu kwa upande wa mmoja
wa wabunge uhuru wao kutohojiwa na inawanyima haki ya kuwahoji au
kuwashitakiwa wabunge wanaotoa kauli zao bungeni hata kama kauli hizo za
wabunge zimevunja haki za wananchi,”alidai wakili Sungusia.
•
Wakili Sungusia
alilitaja dai la pili kuwa ni kuiomba mahakama hiyo itamke kuwa kauli ya Waziri
Mku, Pinda ambayo ililitaka Jeshi la Polisi kuwapiga wale wote wanaokiuka amri
za jeshi hilo, kama kauli hiyo nayo inalindwa na kinga iliyowekwa katika Ibara
ya Ibara ya 100(2) ya Katiba ya nchi ambayo inasomeka hivi:
‘Bila ya
kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge
yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo
lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta
Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.’
Katiba mkutano wa bunge uliomalizika hivi
karibuni , Waziri Mkuu Pinda akiwa ndani ya bunge aliliagiza jeshi la polisi
kuwapiga wale wote wanaokaidi amri za jeshi hilo, kwasababu serikali
imeshachoshwa na vitendo vya baadhi ya wananchi wanaokaidi kwa makusudi amri za
jeshi la polisi , kauli iliyoleta mhemko kwa jamii huku wengine wakiipinga
utekelezaji wa agizo hilo na wengine wakiunga mkono, hali iliyosababisha
LHRC hivi karibuni ilizungumza na waandishi wa habari
wakimtaka Pinda afute kauli yake hiyo ama sivyo watamfikisha mahakamani.
Tanzania Daima.
0 comments:
Post a Comment