Gideon Mwakanosya, songea.
BARAZA la madiwani la halmashauri ya manispaa ya Songea
mkoani Ruvuma wameiomba serikali ichukue hatua za kisheria kwa kampuni ya
Mohamed enterprises tawi la songea sambamba na kuwalipa fidia baadhi ya
wakulima ambao walinunua mbolea inayosadikiwa kuwa ni feki kwenye maduka yake
yaliyopo mjini humo na kuwasababishia hasara wakulima hao katika msimu wa
kilimo uliopita 2012/13.
Ombi hilo limetolewa kwenye kikao cha baraza la
madiwani kilchofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo
ambapo pamoja na mambo mengine madiwani hao walimtaka meya na mkurugenzi
kutoa maelezo yanayojitosheleza kwenye baraza hilo juu ya hatua ambazo
zimechukuliwa kwa kampuni Mohamed Enterprises ambapo ilidaiwa kuwa wamekamata
mbolea feki na bado zipo hadi sasa kwenye maghala yake bila kuteketezwa jambo
ambalo ni hatari.
Akizungumza katika baraza hilo Diwani wa kata ya Ruhuwiko
Gerad Ndimbo alisema kuwa anashangazwa mbolea hiyo feki haijateketezwa hadi
sasa kwa kuwa kisheria na utaratibu ilibidi iteketezwe mara tu baada ya
kukamatwa.
Alisema kuwa kwa jinsi anavyowafahamu wananchi wanaweza
kununua mbolea hiyo kwa bei ya chini na ikaharibu ardhi na kufafanuwa kuwa kwa
sasa mbolea hiyo ni sumu hivyo haikutakiwa iwepo hadi sasa na cha kushangaza ni
kwamba mbolea hiyo hajulikani ipo kiasi gani kwenye maghala.
Katika hatua nyingine Diwani wa kata ya Bombambili kupitia
Chadema Keni Mbangala alilitaka baraza kuahirishwa na kwenda kukagua maghara ya
kampuni hiyo ili kujionea ukweli wa sakata hilo na kuepusha wananchi kuendelea
kutumia mbolea feki.
Nae Diwani wa kata ya Msamala kupitia CCM Kharifa Mgwasa
alisema kuwa jambo hilo kwa sasa ni kero na wanaopata hasara ni wananchi wao
serikali iisifanyie mzaa ni vyema sasa ikachukuwa hatua za kisheria pamoja na
kuifungia kampuni hiyo kuingiza mbolea kwa imeshaleata madhara kwa wananchi.
“Kwa kuwa leo kwenye kikao chetu mkuu wa Wilaya yupo na yeye
kama serikali hatueleze kupitia baraza hili ni hatua gani ambazo
wameshazichukuwa hadi sasa kwa kuwa hawa wakina mohamedi ni wafanyabiashara na
wanamakampuni makubwa hapa nchini bila kuwabana watakao umia ni ni
wananchi wetu.”alisema Mgwasa.
Kwa upande wake Meya wa halmashauri ya manispaa hiyo Charles
Mhagama alisema kuwa wao kama halmashauri hawana uwezo wa kuibana hiyo kampuni
shauri hilo kwa sasa lipo mkoani hawezi kujibia chochote kwa kuwa wanasubiri
majibu lakini kwa kuwa mkuu wa Wilaya yupo kwenye kikao ni vyema akatolea
ufafanuzi juu ya tuhuma hizo.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya hiyo Joseph Mkirikiti alieleza
kuwa suala hilo lilishafanyiwa utafiti wa kina na mwenye kampuni akapewa nafasi
ya kujitetea na serikali ikachukuwa sampo ya mbolea hiyo kwenda kuifanyia
utafiti tena na kuipima kama inafaa kwa matumizi ya kilimo.
Aidha mwakilishi wa kampuni hiyo mkoani Ruvuma Sadiki Mpemba alipohojiwa
na waandishi wa habari kuhusiana na tuhuma hizo aliwaporomoshea matusi
waandishi wa habari na kudai kuwa hafanyii kazi za majungu za wanasiasa
pamoja na waandishi.
0 comments:
Post a Comment