Barack Obama - Rais wa Marekani.
Marekani na Uingereza zimeonyesha
kukerwa baada ya matokeo rasmi ya uchaguzi wa Zimbabwe kumpa ushindi Rais Robert Mugabe ambaye anakamata Ikulu
ya nchi hiyo kwa mara ya sana, huku kukiwa na tuhuma za udanganyifu katika
uchaguzi huo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani
John Kerry amesema matokeo hayo hayawakilishi matakwa halisi ya wananchi wa
Zimbabwe.
Hata hivyo Afrika Kusini, ambayo
ndiyo nchi yenye nguvu zaidi katika ukanda ule, umempongeza bwana Robert Mugabe
kwa ushindi wake.
Bwana Mugabe, mwenye umri wa miaka
89,ameshinda asilimia 61 ya kura zilizopigwa,dhidi ya asilimia 34 ya bwana
Morgan Tsvangirai wa MDC.
Kiongozi wa upinzani nchini Zimbawe
bwana Morgan Tsvangirai amesemA chama chake hakitafanyakazi na chama za Zanu -
PF na kitasusia taasisi za Kiserikali.
0 comments:
Post a Comment