Mabingwa wa
ligi kuu Tanzania bara Yanga African jana Waliibuka na ushindi wa magoli 3-1
dhidi ya mtibwa sugar ya morogoro kufuatia mchezo mkali uliokuwa wa kujipima nguvu
uliokuwa umefanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya
maandalizi ya ligi kuu ya Vodacom inayotaraji kuanza kutimua vumbi Agost 24
mwaka huu.
Mabao ya
yanga yalitiwa kimiani na saidi Bahanuzi katika dakika ya 25 ya kipindi cha
kwanza huku bao la pili likifungwa na Jerson Tegete kwa mkwaju wa Penati katika
dakika ya 81 na bao la tatu liliwekwa kimiani na Hussein Javu kwenye dakika ya
87 ya mchezo
Bala kufutia
machozi kwa upande wa Mtibwa lilifungwa na Shaaban Kisiga kwa njia ya mkwaju wa
penalty na hivyo hadi mwisho wa mtanange huo Matokeo yakawa yanahesabika 3 -1.
Kitu Pekee
ambacho yanga walionekana nacho uwanjani hapo baada ya mchezo ni pale walipo tumia mwanya huo kuwatambulisha
wachezaji wao wapya akiwemo Hussein Javu, Mrisho Ngassa, Rajab Zahir, Hamisi
Thabit, Shaaban Kondo pamoja na Deogratius Mushi Maarufu kwa jina la Dida.
0 comments:
Post a Comment