Mwanaume wa nchini Kenya ambaye aliridhia kusaini mkataba wa
kuchangia mwanamke mmoja na mwanaume mwenzake amefukuzwa kazi na bosi wake.
Mwanaume huyo Sylvester Mwendwa, ambaye mwishoni mwa wiki
alitangaza hadharani penzi lake hilo la mkataba na mwanamke mjane, amesema bosi
wake amemfukuza kazi ya bucha aliyokuwa akiifanya baada ya kusikia habari hiyo.
Mwendwa ambaye alikiri kuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanamke
huyo na yuko radhi kufanya lolote ili aendelee kuwanae hata ikibidi kuchangia
na mwanaume mwingine, amedai amekuwa akipokea ujumbe wa kutishiwa maisha yake.
Baada ya uhusiano wake na mwanamke huyo Joyce Wambui pamoja na
mwanaume mwingine kujulikana kwa umma Mwendwa sasa amelazimika kukimbilia mafichoni
akihofia usalama wa maisha yake.
0 comments:
Post a Comment